Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada watakiwa kwa ajili ya wakimbizi wa ndani nchini Ethiopia; UNHCR

Mkimbizi wa ndani IDP sehemu za Kercha,Zoni ya Guju Magharibi.
OCHA/ Tinago Chikoto
Mkimbizi wa ndani IDP sehemu za Kercha,Zoni ya Guju Magharibi.

Msaada watakiwa kwa ajili ya wakimbizi wa ndani nchini Ethiopia; UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Kufuatia mzozo wa hivi karibuni Kaskazini Magharibi mwa Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR), limetambua haja ya ufadhili wa dharura ili kuitikia mahitaji ya maelfu ya Waitiopia waliolazimika kukimbia makwao ili kuokoa maisha.

Katika mkutano na wandihi wa habari kwenye Palais des Nations mjini Geneva, Uswisi,  Msemaji wa UNHCR, Babar Baloch amesema wanahitaji dola milioni 21.5 ili kuwawezesha kuendeleza usaidizi wa kuokoa maisha kwa wakimbizi hao wa ndani katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Tangu April mwaka huu watu takribani milioni moja wamekimbia makwoa kutokana na vurugu baina ya jamii za mpakani za Southern Nations, Nationalities, Peoples’ Region na Oromia Region.

Vurugu hizo zilitanda wakati nchi hiyo ilmemaliza karibu mwaka mmoja ikikumbana na ukame na mikwaruzano juu ya rasilimali.

Bwana Baloch amesema zaidi ya watu laki mbili waliorejea nyumbani wamekuta miundombinu kama shule, hospitali na ofisi vikiwa vimebomolewa kiasi au kubomolewa kabisa, huku maelfu wakiwa wanahifadjiwa katika miundombinu hizo za umma. Wathirika wengine wanahitaji msaada ya kuokoa maisha ikiwemo chaula, maji, malazi na blanketi.

Hat hivyo kwa kuitikai mahitaji yao, UNHCR inazambaza vifaa  elfu hamsini ikiwemo blaketi na viirago na tayari vifaa 17,400 vimetolea, ufadhili kutoka kwa mfuko wa ufadhili wa dharura wa Umoja wa Mataifa.