Pongezi India kwa kutetea jamii ya LGBTI:UNAIDS

6 Septemba 2018

Mahakama kuu nchini India imetengua baadhi ya vifungu katika sheria za makossa ya jinai nchini humo hususan  kifungu namba 377  kinachoharamisha kundi la watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, LGBTI. Uamuzi huo umepongezwa na taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kupitia mtandao wakewa Twitter, amesema anaunga mkono uamuzi wa leo wa mahakama kuu ya India ,akinukuu baadhi ya maneno ya jaji mkuu Misra kuwa  ubaguzi na upendeleo wakati mwingine havizingatiwi, havipewi uzito, havitetewi na huonekana kama ni kawaida.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na  masuala ya  UKIMWI UNAIDS, Michel Sidibe, amesema  leo ni  siku ya kusherehekea, siku ambayo heshima na hadhi vimerejeshwa India kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, waliobadili jinsia zao,na  walewanaofanya mapenzi na watu wa jinsia zote.

Pia amewapongeza wanaharakati aliowaita majasiri, asasi za kiraia na wote waliotoa mchango wa kufa na kupona ili kuhakikisha udhalimu huo unaondolewa.

Nayo ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini India imefurahia uamuzi huo ambaouliobadilisha kifungu cha sheria ambacho kilianza kutumika enzi za ukoloni na kikiilenga jamii  ya watu wanaofanya mapenzi ya ya jinsia moja na wengineo wa jamii ya LGBTI.

Kwa mujibu wa takwimu nchini India maambukizi ya VVU miongoni mwa wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja  ni aslimia 2.7 na miongoni mwa wale waliobadili jinsia ni asilimia3.1 ikilinganishwa na idadi ya kitaifa ya maambukizi kwa watu wazima ambayo ni asilimia 0.2.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter