Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa ngazi ya juu wamulika masuala ya wanawake, DRC

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa.
MONUSCO/Myriam Asmani
Mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

Ujumbe wa ngazi ya juu wamulika masuala ya wanawake, DRC

Wanawake

Ujumbe wa pamoja kwa ajili ya kutetea masaula ya wanawake umetoa taarifa baada ya ziara yake ya siku nne nchini Jamhuri ya Kidemokrasai ya Kongo, DRC ilioangazia zaidi masuala ya wanawake.

Ujumbe huo umejumwisha mafisa wa Shirika la Umoja wa Matiafa la masuala ya wanawake-UN –Women, Muungano wa Africa (AU) na Ushirika wa Kimataifa kuhusu masuala ya Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR.

Katika ziara yao ilionaza tarehe 16  hadi 19 Agisti wmaka huu, wameafikiana kushikamana katika kupigania haki za wanawake nchini DRC.

Ilifanywa kupitia Bodi ya Ushauri wa mwongozo wa jukwa la wanawake kwa ajili ya amani na usalama, PSCF0.

Ujumbe huo uliaongozwa na Bi. Catherine Samba-Panza, Rais wa muda wa zamani wa Jamhuri ya Africa ya Kati , akisindikizwa na Balozi Liberata Mulamula, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa ICGLR, wote wakiw ani wanachama wa kamati ya mashauriano ya jukwa la wanawake kwa ajili ya amani, usalama na mwongozo wa ushirikiano la DRC, na eneo zima la Maziwa Makuu kwa ujumla.