Bei ya vyakula duniani haikubadilika sana mwezi Agosti: FAO

6 Septemba 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetoa taarifa mpya kuhusu bei ya vyakula kwa mwezi Agosti na kusema  bei kwa ujumla ilibaki palepale, haikuongezeka wala kupungua.

Katika taarifa iliyotolewa leo mjini Roma Italia, FAO inasema  bei ya vyakula  mwezi Agosti haikubadilika sana  kutokana na utabiri uliyofanywa  mwezi  Julai ijapokuwa ilikuwa asilimia 5.4 chini ya kiwango cha  mwezi kama huo mwaka jana 2017.

Bei ya nafaka katika kielelezo cha bei ya vyakula ya FAO, ilipanda kwa asilimia 4.0 mwezi huo, ambapo bei ya ngano ilipanda mara dufu kutokana na kilichoelezwa kama kupungua kwa matumizi katika Umoja wa Ulaya na Urusi. Bei  ya mahindi katika soko la kimataifa  ilipanda kwa zaidi ya asilimia tatu huku bei ya mchele ikapungua  katika mwezi huo.

Sukari nayo ilishuka bei kwa asilimia 5.4 katika mwezi wa Julai bei ambayo ni ya chini kabisa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hii inasemekana imesababishwa na kushuka kwa thamani ya pesa za mataifa ambayo huzalisha na huuza nje sukari hasaBrazil na India.

Kuhusu uzalishaji wa mazoa  utakavyokuwa hapo baade FAO inatabiri kuwa  uzalishaji wa nafaka duniani katika mwaka wa 2018 utafika  tani milioni 2,587, ikiwa ni ongezekokutoka makadirio ya Julai. Hata hivyo inaonyesha kuwa ni kiwango cha chini kikilinganishwa na kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ingawa ni asilimia 2.4 chini ya kiwango cha juu zaidi cha mwaka uliopita.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter