Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 150 hufanyiwa ukatili na kunyanyaswa kila mwaka mashuleni:UNICEF

Hawa ni wasichana watatu wa Progreso, Yoro, Honduras, umri wao ni miaka 13, hadi 14. Ni marafiki na waathirika wa unyanyasaji shuleni.
UNICEF/Adriana Zehbrauskas
Hawa ni wasichana watatu wa Progreso, Yoro, Honduras, umri wao ni miaka 13, hadi 14. Ni marafiki na waathirika wa unyanyasaji shuleni.

Watoto milioni 150 hufanyiwa ukatili na kunyanyaswa kila mwaka mashuleni:UNICEF

Utamaduni na Elimu

Ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, inasema nusu ya wanafunzi wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 15 duniani kote -sawa na watoto milioni 150 - wanaripoti kuwahi kunyanyaswa na wenzao shuleni.

Ripoti hiyo iliyopewa jina, Somo la Kila siku: #KomeshaUkatili katika Shule inasema kuwa unyanyasaji wa rika unaopimwa kwa idadi ya watoto wanaoripoti kunyanyaswa mwezi uliopita au wamehusika katika ugomvi mwaka jana ni sehemu ya matukio katika maeneo ya masomo duniani kote na inaathiri elimu na maisha katika nchi tajiri na hata zile maskini.

"Elimu ni ufunguo wa kujenga jamii za amani, na bado, kwa mamilioni ya watoto duniani kote, shule si salama," amesema Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Henrietta Fore. Akiongeza kuwa "Kila siku, wanafunzi wanakabiliwa na hatari nyingi, ikiwa ni pamoja na mapigano, shinikizo la kujiunga na makundi, unyanyasaji  wa ana kwa ana  na pia mtandaoni, unyanyasaji wa kijinsia na vurugu za kutumia silaha.”

Kwa muda mfupi hii inaathiri mafunzo yao, na kwa muda mrefu hii inaweza kusababisha msongo wa mawazo, wasiwasi na hata kujiua. Vurugu ni somo la kukumbukwa ambalo hakuna mtoto anayestahili kujifunza.”

Ripoti hiyo inaelezea njia mbalimbali ambazo wanafunzi za kuwanyanyasa wanafunzi hao ikiwemo darasani:

Kote duniani, zaidi ya mwanafunzi mmoja kati ya watatu wenye umri wa miaka 13 hadi 15 wamewahi kunyanyaswa , na kiasi kama hicho pia kuumizwa kimwili.

 

Huko Villanueva, Honduras, Darwin,16, anakaa ndani ya darasa alilokuwa akichangia na rafiki yake henry aliejiuwa Septemba 2016. Mwalimu anasema rafiki wa karibu walinyanyaswa na wanafunzi wenzao.
UNICEF/Adriana Zehbrauskas
Huko Villanueva, Honduras, Darwin,16, anakaa ndani ya darasa alilokuwa akichangia na rafiki yake henry aliejiuwa Septemba 2016. Mwalimu anasema rafiki wa karibu walinyanyaswa na wanafunzi wenzao.

Wanafunzi watatu kati ya 10 katika nchi 39 zilizoendelea wanakubali kuwahi kuwanyanyasa wenzao wa rika lao.

Mnamo 2017, kulikuwa na mashambulizi 396 yaliyoandikwa au kuthibitishwa kwenye shule za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, 26 katika shule za Sudan Kusini, mashambulizi 67 katika Jamhuri ya Kiarabu ya Syria na mashambulizi 20 huko Yemen.

Karibu watoto milioni 720 wenye umri wa kwenda shule wanaishi katika nchi ambako adhabu ya kisheria shuleni haizuiwi kikamilifu.

Wakati wasichana na wavulana wako katika hatari sawa ya kudhalilishwa, wasichana wana uwezekano mkubwa wa kuwa waathirika wa unyanyasaji wa kisaikolojia na wavulana wanakabiliwa na hatari zaidi ya unyanyasaji wa kimwili na vitisho.

Somo la Kila siku: #Komesha Ukatili katika Shule hutolewa kama sehemu ya kampeni ya kimataifa ya UNICEF #KomeshaUkatili. Pia ni sehemu ya jitihada za pamoja za kutoa nuru na kuchukua hatua kwa #KomeshaUkatili ndani na karibu na shule na mashirika ikiwa ni pamoja na UNICEF, Idara ya Uingereza inayohusika na Maendeleo ya Kimataifa (DFID), UNESCO, wanachama wengine wa Ushirikiano wa Kimataifa wa kudhoofisha Vurugu Dhidi Watoto na UNGEI. 

Victor Fernando, 17, anasimama karibu na dirisha nyumbani kwake Villanueva, Honduras,Agosti 31,2018. Victor Fernando alinyanyaswa shuleni kutokna na mwelekeo wake wa masuala ya kujamiana.
UNICEF/Adriana Zehbrauskas
Victor Fernando, 17, anasimama karibu na dirisha nyumbani kwake Villanueva, Honduras,Agosti 31,2018. Victor Fernando alinyanyaswa shuleni kutokna na mwelekeo wake wa masuala ya kujamiana.

 

Ili kukomesha unyanayasaji shuleni, UNICEF na washirika wake wanatoa wito  wa hatua za haraka kuchukuliwa katika maeneo yafuatayo:

· Kutekeleza sera na sheria kulinda wanafunzi shuleni.

· Kuimarisha hatua za kuzuia matukio kama hayo shuleni.

UNICEF inawahimiza vijana duniani kote kupaza sauti zao kupitia kapmeni ya #KomeshaUkatili katika shule