Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Acheni kupuuza haki za uzazi za wanawake na wasichana: UN

Moja wa vikao vya wajumbe  wa kamati ya kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW. Kamati hiyo imelaani hatua ya kupuuza haki za uzazi wa wanawake.
UN

Wanawake

Hali ya kupuuza na kutoheshimu misingi ya kimataifa ya haki za binadamu kunatishia  haki za afya ya uzazi na kujamihiana kwa wanawake mkiwemo wenye ulemavu.

Onyo hilo limetolewa leo mjini Geneva Uswisi na wataalam wa masuala ya haki za binadamu.

Hali ya kupuuza na kutoheshimu misingi ya kimataifa ya haki za binadamu kunatishia  haki za afya ya uzazi na kujamihiana kwa wanawake mkiwemo wenye ulemavu.

Onyo hilo limetolewa leo mjini Geneva Uswisi na watalaam wa masuala ya haki za binadamu.

Katika taarifa ya pamoja ,kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake, CEDAW na kamati ya haki za watu wenye ulemavu CRPD, wamesema kuwa kuweza kupata fursa na huduma salama za utoaji mimba  na huduma zingine zinazoambana na hali hiyo na habari kkuhusu suala hilo ni muhimu sana  katika afya ya uzazi kwa wanawake.

Wameongeza kuwa kupata huduma kama hizo ni wajibu  katika kulinda  haki na maisha vya wanawake ,afya kwa jumla , usawa wa kisheria, kutobaguliwa, kupata habari, faragha na uhuru dhidi ya kuteswa na manyanyaso..

Mwenyekiti wa CRPD,Theresia Degener, amesema “Nina wasiwasi  na  wapinzani wa haki za  afya ya uzazi ambao kawaida, hutumia  haki za watu wenye ulemavu katika juhudi za  kuwazuia wanawake kupata huduma salama za kutoa mimba.”

Amesema huku ni kutafsiri vibaya mkataba  kuhusu haki za watu wenye ulemavu. Amefafanua kuwa haki za watu wenye walemavu na usawa wa kijinsia ni vitu viwilivinavyopigania haki chini ya mkataba wa kimataifa na visichukuliwe kama vinagongana.

Mwenyekiti wa CEDAW, Daila Leinarte, kwa upande wake amesema hili ndilo suala nyeti ambalo lina waathiri wanawake wa wasichana hususan  wenye ulemavu. Ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa wanawake wanapata huduma za afya ya uzazi bila ubaguzi wowote ule.