Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani, demokrasia na mustakabali wa Nicaragua viko njia panda:UN

 Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
UN /Loey Felipe
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Amani, demokrasia na mustakabali wa Nicaragua viko njia panda:UN

Amani na Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana Jumatano kenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kujadili hali ya Nicaragua kwa ombi maalumu la Marekani licha ya  upinzani wa kufanya hivyo kutoka kwa Urusi, China, Bolivia na Ethiopia, ambao hawadhani hali nchini Nicaragua ni tishio la amani ya kimataifa.

"Hali ya vifo, machafuko, ukandamizaji, mgogoro wa kisiasa na kijamii Nicaragua ni suala linalotia hofu kubwa Magharibi mwa dunia amesema mkuu wa secretariat ya mashirika ya Amerika ya Kusini (OAS) wakati akihutubia baraza la Usalama na kuonyesha kuwa wanafualatilia hali nchini humo kila wakati.

Gonzalo Koncke amesema tangu Aprili 18 mwaka huu watu 322 wamekufa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ttume ya haki za binadamu ya mataifa ya Amerika na kuongeza kuwa

“"Waathirika hao ni matokeo ya ukandamizaji, vurugu, vitendo vya makundi yenye silaha yanayounga mkono serikali na ukiukwaji wa haki za binadamu," Ameongeza kuwa ripoti ya tume hiyo iliyotolewa Juni 22 inaonyesha kuwa Nicaragua imekiuka haki nyingi za msingi kwa raia wake na kwamba matokeo ya uchunguzi wa ukiukwaji huo yanaiharamisha serikali.

 

Maandamano ya wanafunzi katika mji mkuu wa Nicaragua, Manama.(picha ya Maktaba)
Artículo 66
Maandamano ya wanafunzi katika mji mkuu wa Nicaragua, Manama.(picha ya Maktaba)

Kwa wakati huu sekretarieti imerejelea mwaliko wake kwa serikali kujiunga na juhudi kwa ajili ya mabadiliko ya masuala ya uchaguzi yanayotarajiwa kukamilika Januari 2019.

Wakati huohuo amekumbusha kwamba kwa mujibu wa Almagro , kuendelea na uchaguzi itakuwa muhimu sana na suluhu ya kweli , na hivyo ametoa wito kwa katika mgogoro wa kidemokrasia wa taifa hilo  na kuitolea wito serikali kujihusisha tena na mazungumzo na upande wa upinzani unaowakilishwa na muungano wa kiraia ambao ulipelekea “muafaka wa kuamianiana baina ya pande hizo.

Amesema “Nicaraqua hivi sasa iko njia panda katika mambo ambayo amani yake, demokrasia na mustakhbali vinayategemea. Tunaelewa ni njia panda ambayo ingeweza kuepukika kwa sababu mfumo wa mataifa ya Amerika una nyenzo ulioziweka bayana kwa Nicaraqua ili kupata suluhu.”

 

Bango moja la sema,"Walikuwa wanafunzi na wala sio  wa halifu". Ni katika maandamano mjini Managua, Nicaragua.
Artículo 66
Bango moja la sema,"Walikuwa wanafunzi na wala sio wa halifu". Ni katika maandamano mjini Managua, Nicaragua.

 

Naye mwakilishi wa asas iza kiraia Félix Maradiaga amezungumzia kuhusu mateso na vitisho vya kuuawa wabnavyovipata watetezi wa haki za binadamu na viongozi wa dini, kufungwa kiholela kwa watu, kuswekwa rumande na mateso kwa raia akionya kwamba “Nicaragua inakuwa nchi isiyo na matumaini.”

Kikao hicho cha Baraza la Usalama kimeitishwa na Marekani ambayo ni raia kwa mwezi huu wa Septemba

Kwa upande wake Nicaraqua, kupitia waziri wake wa mambo ya nje  Denis Moncada iliingilia na kusema kwamba kuna muafaka kwenye Baraza la Usalama kuwa nchi yake haitoi vitoisho vyovyote kwa amani na usalama wa kimataifa.