Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi imekiuka haki za binadamu kwa kiasi kikubwa-UN

Doudou Diène, rais wa tume ya uchunguzi Burundi
Picha: UN/Jean-Marc Ferré
Doudou Diène, rais wa tume ya uchunguzi Burundi

Burundi imekiuka haki za binadamu kwa kiasi kikubwa-UN

Haki za binadamu

Tume ya uchunguzi ya Umoja wa mataifa iliyopewa jukumu la kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi, imesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, nchini humo ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu, kati ya mwaka 2017 na 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo  mjini Geneva Uswis, , Francoise Hampson, mjumbe wa tume hiyo ya uchunguzi (COI) Burundi, amesema kwamba "tunapozungumzia ukiukwaji wa haki za binadamu na kuendelea kwa ukiukwaji, tunazungumza juu ya yafuatayo: mauaji ya kiholela, kukamatwa kiholela na kufungwa, vitendo vya mateso na ukatili mwingine, matendo yasiyo ya kibinadamu au dharau, unyanyasaji wa kijinsia, ukiukwaji wa uhuru wa kiraia, ukiukwaji wa haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kwa watu kutoweshwa Hampson ameongeza "haya ni ukiukwaji tuliouona mwaka jana, lakini tuna habari kuhusu kuendelea kwa ukiukwaji huu mwaka 2017 na 2018."

Mazoea mapya, kama kuharibu miili au kufanya matukio nyakati za usiku, hufanya kwa ujumla mauaji kuonekana yamepungua ikilinganishwa na 2015, ameonya.

Hampson akisema "mabadiliko ni kwamba sasa nyakati za usiku watu wanakuja kuwachukua wale wanaowataka na kisha hatupati miili yao tena. Hiyo haimaanishi kwamba hawakufa lakini hatujui wapi tunaweza kuwapata watu hawa "Pengine wanatupwa katika makaburi ya pamoja  au katika mito au labda kuzikwa kwenye magereza. Hii ni kusema kwamba mauaji ya kiholela hayafichwi tena kuliko ilivyokuwa kabla, lakini pia haimaanishi kwamba hayakufanyika. "

"Pengine wanatupwa katika makaburi ya pamoja  au katika mito au labda kuzikwa kwenye magereza. Hii ni kusema kwamba mauaji ya kiholela hayafichwi tena kuliko ilivyokuwa kabla, lakini pia haimaanishi kwamba hayakufanyika. "

Miaka kumi baada kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005, Burundi ilikumbwa na mgogoro mpya mwaka wa 2015 wakati Rais Pierre Nkurunziza aliposhiriki katika uchaguzi kwa muhula wa tatu hali iliyoanzisha maandamano ya wafuasi wa upinzani. Vurugu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu zimeendelea tangu wakati huo.

Mwaka huu, Serikali ya Burundi imekataa, kama ilivyofanya awali, mazungumzo yoyote na tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa. Matokeo ya uchunguzi wa tume hiyo yametokana na maelezo ya waathirika 900 wa ukiukwaji wa haki za binadamu, mashahidi, ikiwa ni pamoja na taarifaza watu 400 zilizokusanywa mwaka uliopita.

Ripoti hiyo imesema kuwa wanachama wa tawi la vijana wa chama tawala, Imbonerakure, wameshiriki zaidi katika ukandamizaji, nje ya mfumo wowote wa kisheria na kwa kulindwa kwa wananchi.

Francoise Hampson amesema "ni nani wahalifu wakuu wa ukiukwaji wa haki za binadamu?" Kama kawaida na kama ilivyokuwa mwaka jana, ni polisi na usalama wa taifa. Ikumbukwe kwamba mwaka huu kuna ushahidi mdogo wa ukiukaji uliofanywa na jeshi. Kwa upande mwingine, kuna vitendo vingi zaidi vinavyotendwa na Imbonerakure ".

Image
Burundi, Agosti mwaka 2015, kwenye mitaa ya Bujumbura. Picha ya Desire Nimubona/IRIN

Tume hiyo imetaka serikali ya Burundi kuwashitaki mawakala wa serikali na Imbonerakure walioshiriki katika ukiukwaji wa haki za binadamu. Tume imebaini kuwa Imbonerakure walitenda waliyoyafanya kwa idhini na udhibiti wa Serikali Burundi.

Hampson ameongeza kuwa "hakuna utaratibu dhidi ya watu wanaofanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Na ni tatizo la kweli, litaendelea kuwa tatizo na litaongeza ugomvi wa kisiasa, kwa sababu hatushughulikii ukiukwaji ambao umefanywa. "

Tume pia inaguswa na kushuka kwa kiwango cha demokrasia pamoja na kuongezeka kwa hali mbaya ya watu. Mgogoro wa kisiasa ambao umeikumba nchi hiyo tangu Aprili 2015 umekuwa na matokeo mabaya  katika  hali ya maisha ya Warundi. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba ukiukwaji wa haki za binadamu uliungwa mkono na wito wa mara kwa mara wa chuki na vurugu, pamoja na Rais wa Burundi.

Tume ya uchunguzi kuhusu Burundi iliundwa septemba 2016 kupitia azimio la Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa na itawasilisha ripoti yake ya hivi karibuni kwenye Baraza la Haki za binadamu tarehe 17 Septemba 2018 mjini Geneva.

Tume hiyo kwa sasa ni njia pekee ya kimataifa ya kuchunguza kwa uhuru ukiukwaji wa haki za binadamu kwa uhuru na haki ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa nchini Burundi, na itaomba kuongezewa muda wa shughuli zake kwa mwaka mmoja zaidi.