Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asimilia kubwa ya watu wameelimika kuhusu Ebola DRC: UNICEF

Afisa wa UNICEF azungumza na watoto kuhusu umuhimu wa kuzuia Ebola karibu na Mangina, Kivu Kaskakzini ,DRC
UNICEF/Mark Naftalin
Afisa wa UNICEF azungumza na watoto kuhusu umuhimu wa kuzuia Ebola karibu na Mangina, Kivu Kaskakzini ,DRC

Asimilia kubwa ya watu wameelimika kuhusu Ebola DRC: UNICEF

Afya

Kampeini ya kuhamasisha Umma kuhusu mlipuko wa Ebola inaendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na takriban watu milioni 2.5 wamefikiwa na kampeni hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF inasema likishirikiana na washirika wake wameweza kuwafikia watu 2,454,000 na ujumbe  wa kujikinga dhidi ya Ebola  tangu ulipozukamlipuko mpya  mashariki mwa DRC.

Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC, Dkt Gianfranco Rotigliano, amesema idadi kubwa ya jamii sasa wana ufahamu kuhusu Ebola Ebola na jinsi ya kujikinga na maambukizi .Na kuongeza “ kujumuisha yamii zilizzo katika hatari ni muhimu sana katika jitihada za kuzuia kusambaa kwa mlipuko.”

Amesema wanashirikiana na jamii hizo kuendeleza  kuendeleza kampeni ya kunawa mikono  na tabia zingine za usafi, kukubali mazishi salama na pia  kutambua na kusaidia watu ambao wanaweza kuwa wameambukizwa na virusi vya Ebola.

Jamii ambazo ziko hatarani zinafikiwa kwa njia mbalimbali kama vile kutumia jamii hizo kuzieleza, mawasiliano ya mmoja kwa moja, ujumbe kupitia redioni, mikutano ya kanisani pamoja na mazungumzo na makundi ya vijana barubaru.

Watu wanane waliopona ugonjwa huo wamejiunga na kampeni ili kuelezea uzoefu wao na kusisitiza  umuhimu wa kutambua mapema dalili za ugonjwa huo na kuwatibu walio na dalili zinazofanana na Ebola.

UNICEF inaendelea kutilia mkazo wa kutoa kipaumbele kwa watoto katika zoezi hili.