Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa ajili ya usalama wao, wakimbizi wa ndani 3500 wahamishiwa kambi nyingine Sudan Kusini:UNMISS

Maelf ya watu waliokuwa wakiishi katika kambi zinazolindwa na UN Juba, Sudan Kusini wamehamishiwa  katika makazi mapya ya muda kambi Mangateen
UNMISS\Nektarios Markogiannis
Maelf ya watu waliokuwa wakiishi katika kambi zinazolindwa na UN Juba, Sudan Kusini wamehamishiwa katika makazi mapya ya muda kambi Mangateen

Kwa ajili ya usalama wao, wakimbizi wa ndani 3500 wahamishiwa kambi nyingine Sudan Kusini:UNMISS

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa umefanikiwa kuwahamisha wakimbizi wa ndani takriban 3,500  kutoka kituo cha ulinzi  wa raia cha Umoja wa Mataifa  mjini Juba hadi na kuwapeleka palipo na usalama zaidi kwa ushirikiano wa  mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini- UNMISS na mashirika ya misaada ya kibinadamu. 

Hapa ni Juba kwenye kituo cha ulinzi wa raia kukiwa na pilikapilika nyingi za watoto wanaingia ndani ya basi kuelekea katika makazi mapya wakati wa zoezi la kuwahamisha.

Nat…

Hatua hiyo inafuatia muafaka wa usitishaji uhasama baina ya makundi mbalimbali kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa katika kipindi cha  wiki kadhaa zilizopita.

Baada ya suluhu kufikiwa  na watu kuonyesha nia ya kuondoka, mashirika ya kibinadamu na UNMISS yalifanya juu chini kuweka makazi ya muda sehemu za Mangateen katikati ya mji.

Sasa mambo yameiva, maafisa wa UNMISS wakiweka hema kubwa ambalo litawahudumia watu hao.Miongoni mwa wajenzi wa hema hilo ni David Shearer, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  na vilevile  mkuu wa UNMISS nchini Sudan Kusini.

“Ilikuwa ni juhudi kubwa  kwa sababu walikuwa wahamishwe haraka kwani tunaamini walikuwa hatarini mahali walipokuwa. Na hii ina maana kuwa kila mtu iimlazimu ashiriki si watoa msaada wa kibinadamu wala walinda amani… na operesheni imekuwa ya mafanikio na kwa muda mmfupi sana.”

Siku chache baada ya kuhamishiwa katika sehemu mpya hali ni shwari kazi zinakwenda barabara huku watoto wakifurahia utoto wao na kukimbia huku na kule.

 

Maelfu ya watu waliokuwa wanaishi katika kambi zinazolindwa na UN Juba wamehamishiwa mahali pengine.
UNMISS\Nektarios Markogiannis
Maelfu ya watu waliokuwa wanaishi katika kambi zinazolindwa na UN Juba wamehamishiwa mahali pengine.

 

Mitaro inachimbwa na wahandishi wa UNMISS, na bomba jipya la maji limewekwa, kituo cha afya kinajengwa.Ingawa maisha ni magumu lakini kuna matumaini.Huyu ni mmoja wa waliohamishwa.

“Yaa tunamatumaini kuwa amani itakuja.Ndio maana tunamwamini kiongozi wetu kutuleta ahapa. Tunamuamini kuhusu amani na kuhusu taifa letu tunadhani litakuwa sawa hapo baadae.”

 Wakati maisha ya kambini baado ni changamoto, angalau  wakimbizi hawa wa ndani wamepigahatua moja mbele ya safari ndefu yenye lengo la kurejea vijijini mwao kuishi salama na maisha yenye hadhi.