Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la Tsunami heri kukinga kuliko kuponya:UNESCO

UN Photo/Evan Schneider
Janga la tsunami ni mfano wa majanga ambayo yaliwahi kutokea Ukanda wa Asia(Picha:

Suala la Tsunami heri kukinga kuliko kuponya:UNESCO

Tabianchi na mazingira

Mataifa 24  likiwemo moja linalopakana na baharí ya Hindi yanashiriki kuanzia leo Jumanne katika zoezi la” wimbi la baharí ya Hindi 2018, au IOwave 2018,” litakalojikita katika hali mbili.

Katika taarifa iliyotolewa mjini Paris Ufaransa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu ,sayansi na utamaduni, UNESCO, matukio mawili bandia ya zoezi hilo, mosi linalofanyika leo 4 Septemba ilhali lingine litafanyika hapo kesho Septemba 5 katika sehemu mbili tofauti.

Tukio bandia la leo litakuwa ni tetemeko la ardhi  la ukubwa wa  9.0 katika vipimo vya ritcher na litatokea  katika mwambao wa kusini mwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo la kesho Septemba 5 litakuwa tetemeko la ukubwa wa 9.3 katika vipimo vya Ritcher litakalotokea katika mwambao wa magharibi mwa Sumatra kaskazini.

 Mazoezi haya yataziwezesha nchi zinazopakana na baharí ya hindi kupata fursa ya  kufanya majaribio ya viwango vya operesheni, mwenendo wa mawasiliano na wadau wote, ambayo ni matayarisho ya Tsunami  na mipango  ya uokozi.

Katika zoezi la mwisho la uokozi mwaka 2016 zaidi ya watu 60,000 walishiriki. Na mwaka huu 2018  Jamii za mwambao ambazo zinapanga kushiriki zoezi la uokozi ni pamoja na shule nchini Comoro, mikoa kadha ya mwambao nchini India; maeneo matano nchini Indonesia ,eneo la mwambao la Makran nchini Iran, kijiji kimoja katika mwambao wa Muscat , Oman, Ushelisheli , Afrika Kusini na Sri Lanka hukuwatutakriban 80,000 watashiriki.

Mataifa yanayopakana na baharí ya Hindi yaliomba kuwekwe mbinu za kutoa tahadharidhidi ya Tsunami kufuatia  janga la Tsunami lamwaka 2004. Mfumo huu ulianzishwa mwaka 2011 kwa ushirikiano na  tume ya UNESCOinayojumuisha serikali mbalimbali na kuhusika na masuala ya baharí IOC.