Ushirikiano wa Afrika na China ni tiketi ya kutomwacha yeyote nyuma:Guterres.

Katibu Mkuu Antonio Guterres ahudhuria mkutano wa kilele wa China na Afrika Beijing Septemba 3, 2018.
Credit: UN China/Zhao Yun
Katibu Mkuu Antonio Guterres ahudhuria mkutano wa kilele wa China na Afrika Beijing Septemba 3, 2018.

Ushirikiano wa Afrika na China ni tiketi ya kutomwacha yeyote nyuma:Guterres.

Masuala ya UM

Ushirikiano baina ya China na bara la Afrika waweza kuwa daraja la kiuchumi la kuhakikisha pande zote zinavuka na hakuna anayesalia nyumba.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, leo akihutubia mkutano  wa ushirikiano kati ya China na Afrika ulioanza mjini Beijing na kusema lengo la jukwaa hilo ni kuchagiza utandawazi uliosawia na kuhakikisha maendeleo endelevu yatakayo mbeba kila mtu na kuchangia katika amani, usalama na pia kujenga, jamii inayojenga mustakabali mwema wa binadamu wote.

 Amesisitiza kuwa “ili kufanikisha malengo hayo, “ushiriki wa wadau wote unahitajika ,hususan serikali, wafanya biashara na mashirika ya ulimwengu wa Kusini kuweza kusaidiana.”

 Akipongeza maendeleo ya kiuchumi ya China na Afrika Katibu Mkuu amesema “China imepiga hatua kubwa za kimaendeleo katika miaka ya hivi karibuni , ikipunguza umasikini kwa kiasi kikubwa na kupongeza nia yake ya kutaka kushirikiana  na mafanikio. Afrika pia imepiga hatua kubwa na ni bara lenye moja ya uchumi wenye mabadiliko makubwa.

 

 

Kwa pamoja amesema China na Afrika zinaweza kujumuisha nguvu zao kwa ajili ya amani, na hatua ambazo ni za kudumu na endelevu. Guterres amesisitiza kuwa “Ni muhimu kwa ushirika wa maendeleo wa sasa na wa baadaye kuchangia katika amani, usalama na ujenzi wa jamii zenye mustakabali wa pamoja.”

Amesema ushirikiano wa maendeleo unaongezeka kwa kuzingatia mambo mawili muhimu :ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya maendeleo endelevu na ajenda ya Muungano wa Afrika ya 2063.Na kupongeza uamuzi huo. Ushirika unaozingatia misingi ya katiba ya Umoja wa Mataifa unaweza kuwanufaisha watu na jumuiya ya kimataifa.

 

Katibu Mkuu Antonio Guterres akitoa hotuba katika mkutano wa kilele kati ya China na Afrika Beijing.
UN China/Zhao Yun
Katibu Mkuu Antonio Guterres akitoa hotuba katika mkutano wa kilele kati ya China na Afrika Beijing.

Jukwaa hili la ushirikiano kati ya China na Afrika  lilianzishwa  Oktoba mwaka 2000 wakati wa mkutano wa mawaziri wa Afrika uliofanyika mjiniBeijing , wanachama wake ni China pamoja na mataifa 53 ya Afrika ambayo yana uhusiano wa kidiplomasia na serikali ya Beijing pamoja na tume ya Muungano wa Afrika.

Bw Guterres ameupongeza  ushirika huo ambao alisema uko katika misingi ya mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuwanufaisha  watu wao pamoja na jamii ya kimataifa kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa UN wa masuala ya uchumi na jamii Liu Zhenmin (kulia) na Balozi wa Kudumu wa China UN Ma Zhaouxu (kushoto) mjini Beijing China.
UN China/Zhao Yun
Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa UN wa masuala ya uchumi na jamii Liu Zhenmin (kulia) na Balozi wa Kudumu wa China UN Ma Zhaouxu (kushoto) mjini Beijing China.

 

Kauli mbiu ya mkutano huu ni: ushirikiano wa ushindi wa pande zote na kufanya kazi pamoja ili kujenga mwelekeo wa jamii ya pamoja kwa nchi ya  China na Afrika, jambo ambalo katibu Mkuu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa amesema linaleta mshikamano ambao ni muhimu kwa mustakbali wa wanaoutaka.

Amesema pia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono ushirika kati ya Afrika na China na pia ule wa  mataifa ya Kusini-Kusini ili mataifa yote yaweze kufaidika na maendeleo endelevu.