Halahala wanachama tushikamane kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina:UN

31 Agosti 2018

Tunasikitishwa na uamuzi wa  Marekani wa kusitisha ufadhili wa fedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA ambalo linawasaidia wakimbizi hao na kuchangia hali ya utulivu katika kanda hiyo, mesema Stephane Dijarric msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika taarifa iliyotolewa Ijumaa.

Katibu Mkuu Antonio Guterres ametoa wito kwa nchi wanachama kushikamana kusaidia kuziba pengo la fedha zilizosalia ili UNRWA iendelee kutoa msaada muhimu na pia matumaini kwa watu hao wa Palestina
Katika taarifa hiyo Dujarric amesema, kwa kawaida Marekani ndio imekuwa mchangiaji mkubwa binafsi wa UNRWA na shirika hilo linashukuru kwa msaada huo wa miaka mingi.

Ameongeza kuwa Katibu Mkuu ana imani kubwa na UNRWA , na kwamba Kamishina mkuu wa shirika hilo Pierre Krahenbuhl, ameongoza kwa kasi juhudi bunifu za bila kuchoka kukabiliana na changamoto ya ufadhili kwa mwaka huu ambayo haikutarajiwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (katikati) Akihutubia mkutano kuhusu hatua za pamoja kusaidia UNRWA
FAO/Pier Paolo Cito
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (katikati) Akihutubia mkutano kuhusu hatua za pamoja kusaidia UNRWA

UNRWA imepanua wigo wa wahisani, kuchangisha kiwango kikubwa cha fedha, na kusaka mbinu mpya za msaada amesema Dujarric akiongeza kuwa, UNRWA pia imechukua hatua madhubuti za kuongeza ufanisi na kupunguza gharama.”UNRWA ina rekodi nzuri ya kutoa elimu bora, afya na huduma nyingine muhimu mara nyingi katika mazingira magumu kwa wakimbizi wa Palestina ambao wana mahitaji makubwa.”

UNRWA ilianzishwa na Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa 1949 ili kutoa msaada na ulinzi kwa watu milioni 5 walioorodheshwa kama wakimbizi wa Kipalestina katika nchi mbalimbali za jirani Mashariki ya Kati. Huduma zake ni pamoja na elimu, misada ya kibinadamu, huduma za jamii, ujenzi na ukarabati wa makambi, huduma za afya na msaada wa dharura.

Mechi ya kirafiki kati ya wafanyakazi wa UNRWA dhidi ya wakimbizi wa Palestina Gaza mapema 2018
UNRWA
Mechi ya kirafiki kati ya wafanyakazi wa UNRWA dhidi ya wakimbizi wa Palestina Gaza mapema 2018

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani, hatua hiyo imefikiwa kwa madai kwamba UNRWA sio shirika halali hojailiyopingwa vikali na msemaji wa UNRWA Chris Gunness ambaye kupitia mtandao wa Twitter ametetea kazi na umuhimu wa shirika hilo na kusema “tunapiga kwa hali na mali ukosoaji wa kwamba shule za UNRWA, vituo vyake vya kiafya na msaada wake wa dharura sio halali.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter