Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu amteua Luteni Jenerali Dennis Gyllensporre wa Sweden kuwa mkuu wa MINUSMA

Meja Generali Jean-Paul Deconinck, Kamada wa MINUSCA anaeondoka.Ameteuliwa kamanda mwingine.
MINUSMA/Harandane Dicko
Meja Generali Jean-Paul Deconinck, Kamada wa MINUSCA anaeondoka.Ameteuliwa kamanda mwingine.

Katibu Mkuu amteua Luteni Jenerali Dennis Gyllensporre wa Sweden kuwa mkuu wa MINUSMA

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo ametangaza uteuzi wa Luteni Jenerali Dennis Gyllensporre wa Sweden kama Kamanda Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani chini Mali MINUSMA.

Luteni Jenerali Gyllensporre anachukua nafasi ya Meja Jenerali Jean-Paul Deconinck wa Ubelgiji, ambaye atamaliza muda wake tarehe 2 mwezi Oktoba. Katibu Mkuu amemshukuru kwa dhati kwa huduma yake nzuri na uongozi wake shupavu kwa MINUSMA.

Kama kamanda Mkuu wa majeshi na pia  mkuu wa vikosi maalamu nchini Sweden tangu Novemba mwaka 2014, Luteni Jenerali Gyllensporre ana uzoefu wa muda mrefu tangu alipojiunga na jeshi la Sweden mwaka 1983. Kati ya mwaka 2008 na 2014, aliwahi kuwa mkuu wa kikosi cha makamanda, mkuu wa Idara ya maendeleo ya jeshi, na pia mkuu wa Idara ya mipango na sera katika makao makuu ya Jeshi la Sweden. Tangu mwaka 2001 hadi 2002, aliongoza kikosi cha 19 cha askari watembea kwa miguu.

Pia ana uzoefu mkubwa wa operesheni za kimataifa, husasan kama afisa mshirikishi nchini Bosnia Herzegovina wakati wa operesheni ya SFOR iliyoongozwa na NATO mwaka 1997-1998, kama naibu mwenyekiti na mkuu wa operesheni katika tume ya pamoja ya kijeshi kwenye milima ya Nuba nchini Sudan kuanzia mwaka 2002 hadi 2003, kama mkuu wa kitengo cha taaluma na dhana katika Jeshi la muungano wa Ulaya huko mjini Brussels, Ubelgiji kuanzia mwaka 2005 hadi 2008, na kama mkuu wakikosi cha Kikanda cha Kaskazini cha ISAF, ambacho kilikuwa ni cha operesheni iliyoongozwa na NATO nchini Afghanistan mwaka 2008.

Luteni Jenerali Gyllensporre ana shahada ya falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Maastricht nchini Uholanzi na stashahada ya uzamivu kutoka taasisi ya kijeshi ya teknolojia nchini Sweden, pia alisoma katika Chuo cha biashara cha Warwick nchini Uiingereza, na Chuo cha Marekani cha makamanda na  majenerali. Yeye pia  ni Profesa msaidizi wa masuala ya mikakati ya kisiasa katika Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Sweden. Pia ni mwanachama wa shule ya sayansi yavita,mjumbe  katika baraza la ushauri wa mashirika ya kiraia ya Sweden, na kwenye bodi ya shule ya Anna Lindh, nchini Sweden.

Luteni Jenerali  Gyllensporre alizaliwa mwaka 1964,  ameoa na ana watoto watatu.