Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa mara ya kwanza mwaka huu watoto 75 waliotumika jeshini waachiliwa Myanmar

Kundi la watoto wanaotumikishwa nchini Myanmar katika jimbo la Kaskazini la Kachin.
PICHA:IRIN
Kundi la watoto wanaotumikishwa nchini Myanmar katika jimbo la Kaskazini la Kachin.

Kwa mara ya kwanza mwaka huu watoto 75 waliotumika jeshini waachiliwa Myanmar

Haki za binadamu

Serikali ya Myanmar kwa mara ya kwanza mwaka huu imewaachilia huru watoto na vijana 75 waliokuwa  wamesajiliwa  na kutumiwa  jeshini na vikosi vinavyojulikana kama Tatmadaw.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Yangon,  Myanmar na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto la UNICEF, inasema hatua hii inasisitiza umuhimu wa kuwalinda watoto katika muktadha wa migogoro ya kivita  na mchakato wa amani.

Mjumbe wa UNICEF nchini  humo ,June Kunugi, amekaribisha hatua hiyo akisema ni moja wa hatua nzuri ya juhudi za serikali zakutaka kukomesha na  kuzuia  Tatmadaw kuwasajili watoto jeshini.

Shirika hilo limeongeza kuwa watoto hao  na vijana waliowaachiliwa leo kutoka jeshini wataingizwa katika mpango wa kujumuishwakatika jamii, na kutumia fursa  hii mpya kujiendeleza na kuchangia kuleta amani nchini Myanmar kama wananchi wazalendo na wenye manufaa kwa taifa lao..

Tangu Juni 2012, wakati  serikali ya Myanmar ilipotia saini kutekeleza mpango wa Umoja wa Mataifa  wa kuzuia usajili na kuwatumia watoto jeshini, watoto na vijana 924 wameshaachiliwa

Wakati wa ziara ya hivi karibuni ya Mwakilishi maalum wa KatibuMkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ya watoto katika migogoro ya silaha,Bi Virginia Gamba, alikutana na maafisa wandamizi kutoka wizara mbalimbali pamoja na jeshi na pia makundi matatu  ya wapiganaji.

Katika mikutano yao aliwaeleza hofu yake kuhusu mwendendo  mpya uliokuwa unajitokeza nchini Myanmar wa ukiukwaji wa haki za watoto nchini kama vile mauaji, ubakaji na kuendelea kuwatumia vitani na kuwatolea wito wa kuwaachilia mara moja watoto hao.