Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafi wa mazingira ni wajibu na jukumu la kila mtu-UNEP

Wakazi wa eneo la ufukwe wa watamu wakifanya  usafi wa ufukwe pamoja  mashirika ya ulinzi wa mazingira
Picha UNEP/Cyril Villemain
Wakazi wa eneo la ufukwe wa watamu wakifanya usafi wa ufukwe pamoja mashirika ya ulinzi wa mazingira

Usafi wa mazingira ni wajibu na jukumu la kila mtu-UNEP

Tabianchi na mazingira

Usafi wa mazingira ni muhimu sana na ni wajibu wa kila mtu, limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maendeleo UNEP.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam nchini Tanzania na mwakilishi wa UNEP nchini humo Clara Makenya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa kwa ajili ya kuunga mkono siku ya kimataifa ya usafi wa mazingira ambayo kila mwaka huwa Septemba 15.

Kwa mujibu wa Makenya, UNEP imeamua kuungana na serikali, asasi za kiraia, mashirika na sekta binafsi kwa sababu ulinzi wa mazingira ni muhimu sio tu maisha na afya ya watu bali pia kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, umasikini na kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s, hivyo amesisitiza

(SAUTI YA CLARA MAKENYA)

“Usafi wa mazingira unachangia kuwa na mazingira bora na mazingira endelevu, hivyo kama shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira hapa Tanzania tunataka kuunga mkono juhudi zote kutoka kwa wadau wote , kuanzia ngazi ya serikali, kwa asas iza kiraia na kwa mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa . Na napenda kutoa wito kwa washirika wetu wote na mashirika ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuchangia na kuunga mkono juhudi hizi zinazoongozwa na jamii nchi nzima.”

Shughuli mbalimbali za usafi wa mazingira zimeambatana na uzinduzi wa kamopeni hiyo ikiwemo washirikli kusafisha ufukwe wa baharí ya Hindi katika eneo la Upanda jijini Dar es salaam.