UNFPA yahaha kushughulikia mahitaji ya wasichana na wanawake, Ufilipino

30 Agosti 2018

Licha ya mzozo kukomeshwa katika nchini Ufilipino,  upatikanaji wa mahitaji ya kibinadamu umesalia changamoto mbele ya wanawake na wasicfana mjini Marawi.

Madhila yanayowakabili ni pamoja na ugumu katika upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na malazi stahiki, mazingira yanayowawia hatari kunyanyashwa na kushambuliwa.

Hata hivyo shirika la Umoja waMataifa la idadi ya watu UNFPA, serikali na wadau  ndio wanatoa matumaini, kwa kuimarisha juhudi za kuwarejesha nyumbani watu waliokuwa wamekimbia mzozo kando na kuwapatia mahitaji ya afya miongoni mwa mengine.

Ikiwa ni miezi tisa baada ya kumalizika kwa mzozo baina ya Serikali na vikundi vilivyojihami, washirika wa wapiganaji wa ISL, uwitikio wa kibinadamu tayari umefanikiwa kurejesha nyumbani watu zaidi ya 320,000, ingawa wengine zaidi ya 70,000 baado wamesalia.

Klaus Beck, Mwakilishi wa UNFPA, Ufilipino amesema kupitia mipango yao kutoa misaada ya afya wanawake na wasichana zaidi ya 2,000 tayari wamenufaika hasa wajawazito,   na kuwapatia taarifa muhimu wakati wa dharura.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter