Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma duni za afya zinatishia hatua zilizopigwa Afrika:WHO

Ripoti kuhusu hali ya kiafya Afrika itatoa hali nzima ilivyo katika bara hilo.
WHO/Africa
Ripoti kuhusu hali ya kiafya Afrika itatoa hali nzima ilivyo katika bara hilo.

Huduma duni za afya zinatishia hatua zilizopigwa Afrika:WHO

Afya

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO kanda ya Afrika iliyotolewa Jumatano ,inaonyesha kuna hatua zilizopigwa katika sekta ya afya barani humo , lakini mafanikio hayo yatakuwa hatarini iwapo nchi hizo hazitaboresha mifumo na jinsi zinavyotoa huduma za afya kwa watu wanaozihitaji zaidi.

Ripoti hiyo “Hali ya afya barani Afrika” inatoa mtazamo wa hali ya afya katika ukanda huo, huduma ambazo watu wanazihitaji, utendaji wa mifumo ya afya na kutathimini mifumo hiyo ina athari gani kwa afya ya watu wa bara hilo.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa mjini Dakar Senegal  kwenye kikao cha 68 cha WHO kanda ya Afrika na Dr Matshidiso Moeti, ambaye mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika  inaonyesha kumekuwa na hakuwa kubwa zilizopigwa katika kuboresha hali ya afya Afrika hasa katika umri watu wanaoishi na muda ambao wanakuwa na afya njema, ukiongezeka kutoka miaka 50.9 hadi miaka 53.8 kati ya mwaka 2012 hadi 2015 ikiwa ni ongezeko kubwa kuliko kanda nyingine yoyote duniani.

Mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa amelala kwenye mikono ya mama yake katika kituo cha afya huko Accra, nchini Ghana
UNICEF/Giacomo Pirozzi
Mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa amelala kwenye mikono ya mama yake katika kituo cha afya huko Accra, nchini Ghana

Hali ya afya Afrika

Pia ripoti inasema kuna mabadiliko katika sababu za magonjwa barani Afrika. Magonjwa yanayoongoza kwa vifo kama ya kupumua, ukimwi na kuhara bado yako kwenye kiwango cha chini na nchi za bara hilo zimejikita katika kuyazuia na kuyatibu na mafanikio yamekuwa makubwa katika kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na maradhi hayo.

Lakini pia vifo vya magonjwa 10 yanayoongoza duniani vimepungua kwa asilimia 50 tangu mwaka 2000 kutoka watu 87.7 hadi 51.1 kwa kila watu laki moja kati ya mwaka 2000 na 2015.

Akizungumzia mafanikio hayo Dr. Moeti amesema “Ninajivunia kwamba Waafrika hivi sasa tunaishi muda mrefu zaidi na tukiwa na afya bora, na tunatumai kwamba mafanikio haya yataendelea na bara letu kufikia viwango vya kimataifa”

Hata hivyo ameonya kwamba huduma ya afya kwa wote zinahitaji kuboreshwa kwa mazingira yote yanayoathiti watu na sio yale ya kipaumbele tu. Maradhi sugu kama saratani yanakatili maisha ya watu wengi zaidi wenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 70 barani Afrikana kufanya mtu 1 kati ya 5 kuwa katika nafasi ya kufariki dunia kutokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs)

Ameongeza kuwa nchi nyingi zinashindwa kutoa huduma stahiki kwa makundi mawili muhimu, vijana barubaru na wazee ambao wanahitaji ,na theluthi moja ya watu waliohojiwa katika utafiti wa ripoti hii wameelezea kutokuwepo kwa huduma kabisa ya wazee katika nchi zao.

Hivyo Dr Moeti amesisitiza “Huduma za afya ni lazima ziende sanjari na mabadiliko na mwenendo katika kanda, tunahitaji kuwa na mtazamo mpya na toshelezi katika afya.”

Image
Picha na: IAEA
Programu ya IAEA ya kudhibiti saratani kwa kutumia mionzi katika nchi za kipato cha chini na cha wastani

Huduma duni za mifumo ya afya

Ripoti pia imebaini kwamba hali ya afya inahusiana na utendaji wa mifumo ya afya katika bara hilo , kukiwa na utendaji mzuri basi kunakuwa na kiwango cha juu cha hali ya afya endelevu na kwa mantiki hiyo mifumo ya afya, watu , taasisi ma rasilimali zinazohitajika kufikisha huduma za afya Afrika utendaji wake ni asilimia 49 tu ya uwezo wake, huku uwezo w anchi kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, ubora wa huduma, mahitaji ya jamii kwa huduma na udhibiti wa maradhi ya milipuko viko chini sana katika bara zima.

Nini kifanyike

Hivyo ripoti imependekeza uwekezaji zaidi katika wahudumu wa afya, na kuwa na kuwa na vituo vya afya karibu na wagonjwa ni muhimu sana katika kuhakikisha fursa lakini kwas asa kuna wahudumu wawili tu na vitanda 15.5 kwa kila wagonjwa 10,000.

Bajeti za sekta za afya barani Afrika ni ndogo na katika nchi 13 watu hutumia chini ya dola 300 kwa masuala ya afya ikilinganishwa na baadhi ya nchi ambako watu hutumia zaidi ya dola 500. Hii inadhihirisha umuhimu wa bara hilo kujikita katika kutafuta suluhu ya jinsi ya kuwekeza katika afya kwani bila kufanya hivyo basi mafanikio yote yaliyopatikana yatakuwa hatarini imesema ripoti hiyo.