Vijana wasanii wana silaha ya kuchagiza haki za binadamu katika jamii zao
Sanaa ni moja ya mbinu inayoweza kutumika katika jamii kufikisha ujumbe na kuchagiza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu ikiwemo lengo la haki za binadamu, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. John Kibego na tarifa kamili
Kwa kutambua mchango wa taalumu ya sanaa , ofisi ya haki za binadamu nchini Tanzania kwa ushirikiano na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es slaam wameendesha mafunzo kwa vijana wasanii wa aina mbalimbali ili kuwachagiza kutumia vipaji vyao kusongesha mbele ajenda ya haki za binadamu katika jamii zao.
Miongoni mwa washiriki ni Hussein Mlele mratibu na mkurugenzi wa shirika la Mulika Tanzania linalohusika na kutoa mafunzo kwa jamii kupityia sanaa ikiwemo afya , elimu ya uraia na haki za binadamu. Anasema mafunzo hayo yamewafungua macho
(HUSSEIN )
Na baada ya kuelima watachukua hatua gani?
(SAUTI YA HUSSEIN )
Hivi sasa Hussein amejumuika na vijana wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na vijana WYFUNA unaoendelea mjini Geneva Uswis .