Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fikra bunifu zinahitajika katika upatanishi wa migogo: Guterres

Mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kudumisha  amani ya kimataifa pamoja na upatanishi wa migogoro.
UN Photo/Evan Schneider
Mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kudumisha amani ya kimataifa pamoja na upatanishi wa migogoro.

Fikra bunifu zinahitajika katika upatanishi wa migogo: Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa vita vinazidi kuwamtihani mgumu, na kupendekeza  juhudi za pamoja, ushirikiano na kuwajumulisha wanawake na vijana katika kuvipatia ufumbuzi..

Guterres ameyasema hayo leo, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York , Marekani  wakati wa kikao cha Baraza la usalama  kilichojadili  mchango wa upatanishikatika kuzuia migogoro. Katika hotuba yake amehimiza  kuwa  kuwepo na fikira bunifu katika suala la upatanishi ni lazima  

“ Ni lazima tlifanye suala la kuzuia kuwa kipaumbele chetu. Na uzuaji huo unajumuisha piakuwekeza katika upatanishi , kuleta amani na ,maendeleo endelevu."

Mkuu huyo wa Umoja wa mataifa  ametaka mashirika kujitolea  kwa kutumia upatanishi kama chombno cha kuokoa  na kuboresha  maisha ya mamilioni  ya watu.

Ameongeza kuwa ana imani inawezekana kushughulikia na kubadilisha mkondo wamigogoro iliyotamalaki sasa kwa hivyo  

‘ Ni lazima tuwe jasiri na wabunifu katika kuleta pamoja mbinu  na uwezo uliopo wa kusaidia upatanishi.”

 Katibu Mkuu pia amesem idadi ya migogo, makundi yaliyojihami kwa silaha na makundi yenye dhamira za kisiasa ambavyo vinafadhiliwa  na magenge ya uhalifu vimechanganyika.

  Amesema inafaa kuwekeza katika suala la upatanishi  na maridhiano kwa kujumisha wadau wote na kutumia nyenzo mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

Kikao hicho kimehudhuirwa pia na  Askofu mkuu wa Cantebury, Justin Welby, kama mwanajopo la Katibu Mkuu la baraza la juu la ushauri kuhusu upatanishi.