Wakimbizi milioni nne wakosa elimu; UNHCR

29 Agosti 2018

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, imesema  watoto wakimbizi zaidi ya milioni nne hawapati fursa ya kuhudhuria shule wakati huu ampapo idadi ya wanaokimbia vita na majanga mengine inaongezeka duniani kote.

Ripoti iliotolewa leo kutokana na utafiti “Badilisha hali sasa elimu ya wakimbizi mzozoni” imebaini kuwa watoto wakimbizi milioni nne hawahudhurii shule, wakti huu ambapo idadi ikiwa imeongezeka kwa laki tano katika mwaka moja pekee.

Hao wakiwa ni asilimia 61 ya watoto wakimbizi wanaohudhuria shule ya msingi ikilinganishwa na 92% ya watoto ulimwenguni kote.

Ripoti Inaongeza kuwa, kuna 23% ya watoto ambao husajiliwa katika shule za sekondari ikilinganishwa na 84% ya watoto duniani kote ili hali wanohudhuria elimu katika tasisi za elimu ya juu ni asilimia 37 pekee.

Pia ripoti inaonyesha hatau zilizopigwa kulekelea mkataba a New York kuhusu wakimbizi na wahamiaji ambayo ni pamoja na kuandikisha wakimbizi wengine 500,000 waliokuwa wameacha shule katika mwaka 2017.  Inachagiza ushirikiano Zaidi na sekta binafsi, wahudumu wa kibidanamu, serikali na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kutafuta suluhisho endelevu kwa changamoto kuhusiana na elimu ya wakimbizi.

Kamishina Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi amesema njia ya kusaidia kufuta machozi ya watoto ni kuwapa elimu  amabyo pia ni muhimu  kwa ujenzi mpya wan chi zao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter