Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zote katika mzozo Yemen zimetekeleza uhalifu

Kijana acheza akipita magofu ya nyuma zilizoharibiwa na mashambulio ya angani katika mji wa zamani wa Saada nchini Yemen
N OCHA/Giles Clarke
Kijana acheza akipita magofu ya nyuma zilizoharibiwa na mashambulio ya angani katika mji wa zamani wa Saada nchini Yemen

Pande zote katika mzozo Yemen zimetekeleza uhalifu

Amani na Usalama

Pande zote katika mzozo unaoendelea nchini Yemen zimetekeleza na zinaendelea kutekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki na uhalifu chini ya sheria za kimataifa na kusababisha zahma kubwa kwa mamilioni ya raia, limesema leo ripoti ya jopo la wachunguzi lililoteuliwa na Umoja wa Mataifa.

Jopo hilo la wataalamu kuhusu Yemen lililoundwa na Baraza la Haki za binadamu limekuwa likichunguza na kuchambua ukiukwaji na ukatili kwa kuzingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu na uhalifu, na limefanya zaira z aidi ya 12 nchini Yemen na mataifa jirani. Miongoni mwa wajumbe wa jopo hilo ni Charles Garraway amesema

"Kundi hili la wataalam lina kila sababu nzuri za kuamini kuwa Serikali za Yemen, Falme za Kiarabu na Saudi Arabia zinahusika na ukiukwaji wa haki za binadamu na jopo pia lina sababu za kuamini kwamba vikosi vya upinzani vinahusika na ukiukaji wa haki za binadamu katika maeneo wanayoyadhibiti,"

Jopo hilo ambalo lime limekusanya ushahidi wake kwa kufanya mahojiano n apande mbalimbali wakiwemo raia nchini Yemen limeangazia hali kuanzia Septemba 2014 hadi June 2018.

Mkutano na waandishi habari wa jopo la wachunguzi lililoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen.Wamechapisha rpoti kuhusu madai ya utekelezaji wa  ukatili.
UN Geneva/Daniel Johnson
Mkutano na waandishi habari wa jopo la wachunguzi lililoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen.Wamechapisha rpoti kuhusu madai ya utekelezaji wa ukatili.

 

Ripoti ya jopo hilo inasema mashambulizi ya anga yanayofanywa na muungano unaoongozwa na Yemen yamesababisha madhara makubwa kwa raia na kulifanya jopo hilo kuamini kwamba mashambulizi hayo ynaweza kuwa uhalifu wa vita.

"Watu binafsi katika serikali ya Yemen na muungano , ikiwemo Saudi Arabia na falme za Kiarabu huenda wamefanya mashambulizi kwa kukiuka kanuni za utofauti, uwiano na / au kiwango, ambacho kinaweza kuwa na uhalifu wa vita,"

Ameongeza kwamba orodha ya maalumu ya majina itawasilishwa kwenye osifi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu ukisubiriwa uchunguzi zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti ya jopo hilo zaidi ya watu milioni 22 bado wanahitaji msaada nchini Yemen na karibu wote ni wanawake na watoto. Mgogoro wa Yemen ulianza 2011 , lakini mapigano yalishika kasi Machi 2015 wakati muungano wa kimataifa unaoonmgozwa na saudí arabia ulipoingilia kijeshi kwa ombi la Rais wa Yemen wakati huo dhidi ya wapigamaji wa Houthi wapinzani wa Rais huyo wa zamani  Ali Abdallah Saleh.