Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utoaji wa misaada ya kuboresha afya ya uzazi uambatane na elimu mahsusi

Mama na mwanae mchanga wakipata huduma baada ya kujifungua kwenye wodi ya wazazi iliyoko kliniki ya Shakawe nchini Botswana.
UNICEF/Christine Nesbitt
Mama na mwanae mchanga wakipata huduma baada ya kujifungua kwenye wodi ya wazazi iliyoko kliniki ya Shakawe nchini Botswana.

Utoaji wa misaada ya kuboresha afya ya uzazi uambatane na elimu mahsusi

Afya

Tanzania imepiga hatua kubwa katika uimarishaji wa afya ya uzazi kufuatia juhudi za pamoja ikiwemo serikali, ambapo serikali imetunga sera rafiki ikiwemo likizo ya uzazi kwa baba mzazi baada ya mke wake kujifungua.

Asia Magoma kutoka Shirika la kiraia la Mmbiki Memorial Foundation ambalo limejikita katika kuimarisha afya ya uzazi, amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kando mwa mkutano wa 67 wa Umoja wa Mataifa na asasi za kiraia uliofanyika jijini New York, Marekani.

Hata hivyo Bi. Magoma amesema licha ya hatua zilizopigwa na uwasilishaji wa misaada kwa ajili ya kuimarisha afya ya uzazi bado kuna pengo.

Aidha Bi Magoma amesema wakati wa kutoa mafunzo licha ya suala la mama mja mzito kuonekana kama jambo la kawaida lakini….