Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyombo vya habari tangazeni habari zinazoinua wanawake-Phumzile

Mtu anarambaza kupitia mitandao ya kijamii.Bi Phumzile avitaka vyombo vya habari kutangaza habari kuhusu wanawake.
World Bank/Simone D. McCourtie
Mtu anarambaza kupitia mitandao ya kijamii.Bi Phumzile avitaka vyombo vya habari kutangaza habari kuhusu wanawake.

Vyombo vya habari tangazeni habari zinazoinua wanawake-Phumzile

Wanawake

Umoja wa Mataifa umetaka vyombo vya  habari nchini Tanzania kupazia sauti habari ambazo zinamnyanyua mwanamke kama  njia mojawapo ya kujenga  uwezo wa watoto wa Kike na wanawake wengine.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN-WOmen, Phumzile Mlambo-Ngucka amesema hiyo jijini Dar es salaam, kando mwa mkutano kuhusu jinsia na masuala ya habari.

Akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo, Bi. Phumzile amesema..

“Watu ambao wanahisi kuwa wameachwa nyuma, kuona watu wanaofanana nao kwenye vyombo vya habari, ni moja ya njia kubwa na rahisi ambayo vyombo vya  habari vinaweza kufanya na kuboresha maisha ya watu. Ninaweza kwenda mahali nikazungumza na vijana kwenye jamii ambayo wameachwa nyuma. Wataniangalia tu! Lakini pindi wakiona mifano ya baadhi ya watu wao ambao ni wanasayansi wabobezi, nao sasa wataamini pindi ninapowaeleza kuwa hata wao wanaweza kuwa wanasayansi.”

Hoja hiyo ikaungwa mkono na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile ambaye amesema ingawa kuna hatua zimepigwa katika uandishi wa habari za masuala ya jinsia, bado kuna vyombo vya habari ambavyo vinajikita katika kuandika habari zilizo na mtazamo hasi kwa wanawake.

Amesema ni vyema kuandika, kuchapisha na kutangaza habari zinazoonyesha harakati za wanawake kujiukwamua na kusema kuwa kuna wanawake wengi waliosonga mbele kimaendeleo na wanaweza kutumiwa kama mifano ili kuchagiza wanawake, wasichana na watoto wa kike.

Mkutano huo wa siku tatu utamalizika Ijumaa.