Teknolojia ya kidigitali ni kivutio cha vijana kwa kilimo: FAO

22 Agosti 2018

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), linaamini kuwa ubunifu wa kidigitali katika kilimo waweza kuchangia pakubwa katika kushirikisha vijana kwa shughuli za kilimo kwa ajli ya mapato na hatimaye kupunguza ukosefu wa ajira miongoni mwao.

Katika makala iliyochapishwa kwenye wavuti wa shirika hilo, FAO inasema vijana wanaweza kupata ajira bora katika kilimo na chakula kwani teknolojia hizo huzusha huduma nyingi kwa wakulima wadogowadogo ambamo vijana waweza kushughulishwa.

FAO imesema ni muhimu teknolojia hizo kukumbatiwa ili kuzuia idadi kubwa ya vijana duniani kote ambao wanachagua kuishi mijini wakisaka kazi za ofisini bila kufahamu kwamba kilimo kina uwezo mkubwa zaidi kupunguza umaskini, kwa kuzingatia mfano wa Afirika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako asilimia 60 ya watu wake bilioni 1.2 ni wa umri wa chini ya miaka 25.

UNICEF/UN070227/Chisiza
Ndege zosizokuwa na rubani (drones) katika baadhi ya maeneo kama nchini Rwanda zinatumika kusambaza dawa katika maeneo yaliyo magumu kufika kwa njia ya barabara.

Tayari FAO imepata mbinu mpya za teknolojia imara katika kilmo ikiwemo ndege zisizo na marubani (drones), na inakadiriwa kuwa kilimo kitakuwa sekta ya pili kuzitumia zaidi katika miaka mitano ijayo na dawa za kutokomeza wadudu aina ya  viwavi jeshi, wanaoharibu mazao.

Teknolojia nyingine ni program ya simu za rununu za kisasa itwayo “Nuru App” inayobaini iwapo dawa za kuuwa viwavi jeshi zimedhuru mazao na apu ya Abalobi inayotumiwa na wavuvi wadogo wadogo kuweka takwimu za samaki waliovuliwa, walipovuliwa na lini wamevuliwa.

FAO imesema matumizi ya teknolojia hizi zote katika kilimo ni chanzo cha ajira zinazovutia vijana.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter