Mazungumzo ya Yemen; serikali na upinzani watumiwa mwaliko
Dalili za kupata suluhu ya mzozo wa Yemen zinaanza kuonekana kufuatia taarifa zinazothibitishwa kuwa Umoja wa Mataifa umewasilisha mwaliko wa mazungumzo kati ya serikali ya Yemen na wanamgambo wa kihouthi tarehe 6 mwezi ujao huko Geneva, Uswisi.
Tangazo hilo lililotolewa leo huko Geneva, Uswisi linakuja baada ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen Martin Griffiths kutangaza tarehe hiyo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapema mwezi huu.
Mzozo wa Yemen umedumu kwa zaidi ya miaka 3 na kusababisha vifo, njaa na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kijamii na raia wengi kusaka ukimbizi ndani na nje ya nchi hiyo.
Mazungumzo haya ya amani yanasonga kufuatia juhudi za pamoja zilizoanzishwa miaka 2 iliyopita chini ya uongozi wa mfalme Sheikh Jaber al-Ahmad al-Sabah wa Kuwait ambaye alijenga msingi wa mazungumzo yanayoendelea hivi sasa .