Urusi muachilieni haraka mtengenezaji filamu wa Ukraine: UN

15 Agosti 2018

Wataalam wa Umoja wa Mataifa  wamezitaka mamlaka nchini Urusi zimuachilie huru mara moja  na bila masharti Oleg Sentsov, huku wakielezea wasiwasi wao kuhusu hali yake ya kiafya kwa sasa.

Olego Sentsov,  mtengenezaji wa filamu raia wa Ukraine na mkosoaji mkuu wa hatua ya Urusi ya kukalia kwa nguvu eneo la Crimea,  alikamatwa mwezi mei mwaka 2014 na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kosa la ugaidi, kama raia wa nchi hiyo.

Kupitia taarifa yao waliyotoa leo mjini Geneva Uswisi, watalaam hao wamesema “maisha ya Sentsov yako hatarini. Mgomo wake aliouanza  unafuatia hukumu ambayo ina mapungufu ya kiwango cha sheria za kimataifa na tunazitaka mamlaka za Urusi zimuachie haraka bila masharti yoyote.”

Miezi mitatu iliyopita alianza mgomo wa  kula chakula akipinga kile anachoamini kuwakufungwa jela kwa raia 64 wa Ukraine nchini Urusi kwa sababu za kisiasa. 

Watalaam wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa  serikali ya Urusi kuhakikisha kuwa, Bwana Sentsov anapewa matibabu anayohitaji haraka na ambayo yanatokana na idhini yake.

Tayari wataalamu hao wanawasiliana na serikali hiyo kuhusu kesi yake hii.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter