Sera za maendeleo na utandawazi hazinufaishi watu wa asili: Dkt Laltaika

9 Agosti 2018

Upanuzi wa miji, migorogo ya kivita ,mabadiliko ya tabianchi  na umasikini ni baadhi tu ya  changamoto zinazosababisha jamii za watu wa asili kuhama makazi yao ya asili  na kutafuta maisha bora nje na ndani ya mipaka yao.

Huo ni ujumbe wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  hii leo katika siku ya kimataifa ya  watu wa asili ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 agosti.

Bw. Guterres amesema kuwa  uhamiaji ni fursa, lakini pia una hatari zake  ambapo wahamiaji wengi wa jamii ya asili wanajikuta wakiishi katika hali zisizo salama na tofauti na mila zao katika maeneo mbalimbali ya miji . 

Ameongeza kuwa wanawake na wasichana wa jamii hizo hukabiliwa  na  aina nyingi za ukatili na unyanyasaji  ikiwemo usafirishaji haramu ambapo vijana wao  wanakabiliwa na changamoto za utambulisho na pia maadili.

Ili kufahamu kwa kina changamoto hizo Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa imezungumza Dkt. Elifuraha Laltaika ambaye ni mtaalamu wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili, ambaye amesema ..

Sauti ya dkt. Elifuraha Laltaika

Na je nini kifanyikie ili jamii hizo ziweza kunufaika?

Sauti ya dkt. Elifuraha Laltaika

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter