CSW yaleta nuru kwa wamasai huko Arusha-Tanzania
Mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliofanyika mapema mwaka huu jijini New York, Marekani umezaa matunda kwa wanawake wa jamii yakimasai mkoani Arusha nchini Tanzania.
Akizungumza kwa njia ya simu na Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Alais Esoto ambaye ni mkurugenzi wa shirika la kiraia la Naserian linalojishughulisha na masuala ya haki na maendeleo kwa wanawake na wasichana wa jamii ya wamasai amesema baada ya kupata mafunzo ya kumkwamua mwanamke kwenye mkutano huo wameanzisha miradi mbalimbali ambayo imekuwa mkombozi kwa makundi hayo.
Sauti ya Alais Esoto
Pamoja na kuwekeza katika elimu ya watoto wa kimasai, bwana Esoto amezungumzia pia mradi wa ufugaji unaosaidia wanawake masikini.
Sauti ya Alais Esoto
Shirika hilo la kiraia la Naserian limekuwa likishirikiana na wadau mbalimbali katika kutokomeza mila mbalimbali ikiwemo ukeketaji wa wasichana na wanawake mkoani Arusha.