Sifahamu utaifa wangu kama ni Burkina Faso au Cote d’Ivoire- Mkimbizi

6 Agosti 2018

Ukosefu wa utaifa umesababisha zaidi ya watu milioni 10 duniani kushindwa siyo tu kuijendeleza kiuchumi bali pia kijamii, imesema ripoti ya mwaka 2017 ya shirika la Umoja wa Mataifala kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Huyu ni kijana Ali, miongoni mwa kundi hilo la watu zaidi ya milioni 10 wasiokuwa na  utaifa, anasema anatambua alizaliwa Abengourou mji ulioko Cote D’Ivoire, lakini hafahamu iwapo anatokea Burkina Faso au Cote d’Ivoire, nchi zilizoko Afrika Magharibi. Ndani ya nchi mbizi hizi kuna watu laki 7.

Nats….

Akizungumza kwenye video ya kampeni ya I Belong au hojiwa wakati wa kampeni ya “I BELONG” au “Mimi Ni” ya UNHCR, Ali anasema hali hiyo ya kutofahamu anatoka taifa gani inamuathiri kiuchumi na kijamii kwani hawezi kufanya chochote.

Ali alitamani kuwa dereva lakini hawezi kuajiriwa bila kitambulisho cha  uraia na hawezi hata kufungua akaunti ya benki.

Sauti ya Ali

Najishikiza  na vibarua vya mashambani kwa kuwa sina jinsi, nilitamani sana kuwa dereva ila kwasababu sina vibali hakuna anayeweza kuniajiri.

Nats…..

Akizungumza kwa uchungu na masikitiko makubwa, Ali anasema..

Sauti ya ALi

Sasa hivi tayari nimetimiza umri wa kuoa, ila bila vibali nitaweza je ? Mpaka sasa hivi nilitegemea angalau niwe na watoto wawili au watatu. Ninachotamani na mimi ni kuwa  na maisha mazuri kama marafiki zangu, na niwe mwenye furaha.

Ili kuondoa vikwazo hivyo vya ukosefu wa utaifa, UNHCR imeazimia kutokomeza madhila hayo ifikapo mwaka 2024 kwa kuelimisha jamii na mataifa juu umuhimu wa kila binadamu kuwa na utaifa.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii