Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanawake wasionyonyesha watoto wao huko Bukoba nchini Tanzania yaongezeka- Takwimu

Mwanamke akimnyonyesha mwanae
UNICEF/Marco Dormino
Mwanamke akimnyonyesha mwanae

Idadi ya wanawake wasionyonyesha watoto wao huko Bukoba nchini Tanzania yaongezeka- Takwimu

Wanawake

Wiki ya unyonyeshaji duniani ikiwa imeingia siku ya tatu, inaelezwa kuwa katika manispaa ya mkoa mmoja kaskazini-magharibi mwa Tanzania idadi ya wanawake wasionyonyesha watoto wao kwenye kipindi cha miezi sita ya mwanzo tangu kuzaliwa imeongezeka na hivyo kuhatarisha uhai wa watoto hao.

Afisa lishe wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera nchini humo Napendaeli Filemon amemweleza Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM kuwa idadi kubwa ya akina mama katika manispaa hiyo hawazingatii umuhimu wa lishe kwa watoto katika miezi ya kwanza ya kuzaliwa na kwamba.

Mahojiano Napendaeli na Nicolaus

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kuwa unyonyeshaji watoto maziwa ya mama punde tu wanapozaliwa kunawakinga dhidi ya magonjwa hatari kama vile Pepopunda, vichomi na kuhara.