Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNISFA yakabidhi kwa utawala mahabusu iliyokarabati Abyei

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa muda kwenye jimbo la Abyei (UNISFA)  ukipiga doria Abyei
IRIN/Hannah McNeish
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa muda kwenye jimbo la Abyei (UNISFA) ukipiga doria Abyei

UNISFA yakabidhi kwa utawala mahabusu iliyokarabati Abyei

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa muda kwenye jimbo la Abyei (UNISFA) umekabidhi kituo cha mahabusu cha polisi wa jamii kilichokarabatiwa na mpango huo kwenye eneo la Ngok Dinka, jimboni humo  nchini Sudan.

Akikabidhi kituo hicho kwa chifu wa Ngok Dinka, bwana Bulabek Deng Kuol mapema wiki hii, afisa mshauri wa polisi wa UNISFA Bi Mary Gahonzile amesema, ukarabati umekamilika vizuri na kituo hicho sasa kina ofisi, vyumba vya mahabusu vinavyowatenganisha wanawake na wanaume na verannda inayoweza kutumika kwa ajili ya mazoezi hali ambayo itasaidia kupunguza msongamano , kuwezesha kuwatambua vizuri na kuwatenganisha mahabusu.

Bi Gahonzire pia amesisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu na kurejea kusema kwa mahabusu inapaswa kuwa mahali pa mafunzo ya kubadili tabia za watu kuliko kuwaadhabisha “kama jamii ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba wafungwa wanapoachiliwa, jamii inafaidika nao.”

Hotuba yake ya makabidhiano ya kituo hicho imeainisha kwamba uongozi wa jamii ufikirie kutowakatia kifungo wahalifu watoto na wenye kesi ndogondogo, kwani jela itawaathiri zaidi endapo watachanganywa na wahalifu wa makossa makubwa kama majambazi na wauaji. 

Naye chifu wa Ngok Dinka amepongeza na kuyashukuru mashirika ya UNISFA husuan shiririka la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa ukarabati wa mahabusu hiyo. Pia ameishukuru polisi ya Umoja wa Mataifa UNPOL, kwa kufikisha shida yao kwa IOM na kuusifu ushauri wa Bi Gahonzire. Kwa upande mwingine chifu huyo ametoa Shukran kwa UNSFA akisema kwa njia nyingi imekuwa ikipigania na kuhakikisha haki za watu wa Abyei ikiwa ni pamoja na mafunzo yanayotolewa na UNPOL kwa polisiwa Abyei.