Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kisiwa cha marashi kiko hatarini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi:UNDP

Wavuvi wakiwa katika shughuliza zao katika visiwa vya Comoro
UNDP Comoros/James Stapley
Wavuvi wakiwa katika shughuliza zao katika visiwa vya Comoro

Kisiwa cha marashi kiko hatarini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi:UNDP

Tabianchi na mazingira

Comoro, ni kisiwa kimesheheni fukwe mwanana, milima ya volkano, manukato ya maua ya ylang-ylang yanayotoa mafuta ya uzuri, lavani au vanila na karafuu, ni kisiwa kilichoko kwenye baharí ya Hindi katikati ya Afrika na Madagascar, kisiwa hiki ni maarufu kama ‘kisiwa cha marashi”

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP Paradiso hii hivi sasa iko njia panda kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayotishia maisha ya watu wanaoendeleza mazoea ya kilimo cha jadi kinachokiweka kisiwa hiki katika hatari kubwa.

Kisiwa hiki ni moja ya visiwa vidogo kabisa na masikini zaidi barani Afrika. Kilimo kinasalia kuwa uti wa mgongo wa maisha ya Wacomoro huku zaidi ya asilimia 30 ya wafanyakazi wa taifa hilo wakipata ujira na kumudu maisha yao kupitia mashamba. Takriban watu 200,000 wanategemea kilimo kwa kila kit na hawa ujuzi wowote katika kilimo, katika wakati huu ambao elimu ya jadi inatoweka , wakulima hawa wanahitaji kuelimishwa, kupata tarifa, na nyezo za kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi  kuliko wakati mwingine wowote .

Kwa mujibu wa UNDP ukosefu wa mbinu za kisasa umewasababishia wakulima wengi hasara kubwa , mtego wa umasikini na kuzuia uwezo wa nchi hiyo kufikia malengo ya kupunguza umasikini, kuwa na uhakika wa chakula na malengo mengine yaliyoainishwa katika ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030.

Njia mojawapo inayotumiwa na serikali kuwasaidia wananchi kukabiliana na hali hiyo ni kupitia mradi wa “  Kuimarisha uwezo wa kuhimili na mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika sekta ya kilimo (CRCCA) . Mradi ambao unafadhiliwa namfuko wa  kituo cha kimataifa cha mazingira kwa nchi zilizo na maendeleo duni (GEF-LDCF) na UNDP. Mradi huo unajitahidi kuhakikisha wakulimanchini Comoro wana uwezo, nyenzo na teknolojia wanayohitaji kupunguza hatari ya m,abadiliko ya tabia nchi kwenye mifumo ya kilimo.

Mradi huo ulioanzishwa mwaka 2014 umeshasaidia karibu jamii 200 za wakulima ambao wako katika hatari ya mabadiliko ya tabia nchi katika kisiwa hicho.