Kuchagiza amani Afghanistan ni wajibu wa kila mwananchi: UN

31 Julai 2018

Kila hatua inayopigwa kuelekea amani nchini Afghanistan ni muhimu sana kwa sasa kulliko wakati mwingine wowote ulee. Wito huo umetolewa leo na  viongozi wa kijamii katika mdahalo unaoungwa unaofanyika mkoa wa Kusini wa Kandahar nchini humo na kuungwa mkono na Umoja wa wenye  lengo la kumulika mbinu za kutanzua mgogoro na kujenga mshikamano wa jamii.

Mdahalo umeandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA kwenye mkoa wa Kandahar kabla ya uzinduzi wa midahalo kadhaa ya redio na televisheni ambayo itaanza hivi karibuni nchini nzima ikijikita na umuhimu wa kutanzua migogoro kwa njia za amani.

Katika moja wa vipindi vya mwanzo vya redio kupitia kituo cha Hewad Radio mjini Kandahar, washiriki wametilia mkazo, umuhimu wa raia wote wa Afghanistan, kuchangia juhudi za kupunguza machafuko  katika ngazi ya jamii.

Mmoja wa washiriki, Khalid Ahmad, ambae ni mjumbe wa baraza la mkoa wa Kandahar amesema kuwa kila mwananchi wakiwemo wanawake , ni sharti wafanye kazi ya kuchagiza amani. Ameongeza kuwa “ amani maana yake ni ari , kupiga hatua na kila mtu kujitoa kujenga taifa lake, lakini kwa bahati mbaya amani haitokuja kirahisi Afghanistan inabidi tufunge mkanda kweli kuipata.”

Duru zinasema wote waliokusanyika kwenye mdahalo na washiriki wa kipindi cha redio wameafiki kuwa  majadiliano na  raia wote wa Afghanistan ndio njia inayofaa kufuatwa  ilikupungza machafuko na wameelezea matumaiani kwamba mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni  ni kama hatua moja kubwa ya kuelekea upatikanaji wa amani ya kudumu nchini humo .

UNAMA ina jukumu la kuisaidia serikali ya Afghanistan na watu wake  katika masuala ya uongozi bora  , kuletya maendeleo, kuunga mkono mchakata wa amani na maridhiano , kulinda haki za binadamu na pia kuwalinda raia dhidi ya  migogoro, utawala bora na kuhimiza ushirikiano wa kikanda.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter