Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaongeza msaada, huku maelfu wakifungasha virago Nicaragua

Waandamanaji mjini Managua katika maandamano ya kudai kukomesha machafuko nchini Nicaragua. Vurugu zimechangaia watu wngi kusaka hifadhi nchi jirani.
Artículo 66
Waandamanaji mjini Managua katika maandamano ya kudai kukomesha machafuko nchini Nicaragua. Vurugu zimechangaia watu wngi kusaka hifadhi nchi jirani.

UNHCR yaongeza msaada, huku maelfu wakifungasha virago Nicaragua

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, leo limetoa wito wa mshikamano wa kimataifa na msaada kwa ajili ya Costa Rica na nchi zingine zinazo wahifadhi wakimbizi na waoomba hifadhi kutoka Nicaragua, wakati maelfu wakifungasha virago kukimbia shinikizo la kisiasa, machafuko na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.

UNHCR inasema katika miezi ya hivi karibuni idadi ya maombi ya raia wa Nicaragua kutaka hifadhi katika nchi jirani ikiwemo Costa Rica yameongezeka kwa kiasi kikubwa. William Spindler ni msemaji wa UNHCR Geneva

(SAUTI YA WILLIAM SPINDLER)

“Hivi sasa kwa wastani maombi 200 ya hifadhi huwasilishwa kila siku nchini Costa rica.  Kwa mujibu wa uongozi wa Costa Rica karibu maombi 8,000 ya hifadhi ya raia wa Nicaragua yameorodheshwa tangu Aprili na mengine , 15,000 yamepewa tarehe ya  kusailiwa baadae kwani mfumo wa uandikishaji nchini humo umezidiwa uwezo.”

 UNHCR inaimarisha uwepo wake nchini Costa Rica kwenye mpaka wa jimbo la Kaskazini na kwa ushirikiano na serikali ya Costa Rica, mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na wadau wasio mashirika ya kiserikali, NGO’s wanaongeza juhudi za kuweza kutoa ulinzi wa haraka na msaada kwa maelfu ya wakimbizi na waoomba hifadhi hao wa Nicaragua ambao wote ni kutoka jimbo la Kaskazini  na maeneo ya katikati yam ji mkuu San Jose.

Wakati Costa Rica wamepokea maombi mengi zaidi , lakini pia Pabana, Mexico na Marekani wameeleza kuongezeka kwa maombi ya raia wa Nicaragua wanaohitaji ukimbizi wa kimataifa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018 na nchi zingine kama Honduras, El Salvador na Guatemala zimekuwa  kituo cha muda kwa wakimbizi na waoomba hifadhi hao.