Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo niliyopata ntahakikisha yaleta matunda Rumbek:Mwangi

Polisi wa Umoja wa Mataifa akiwa na watoto. (Picha/UNPolice)

Mafunzo niliyopata ntahakikisha yaleta matunda Rumbek:Mwangi

Amani na Usalama

Maafisa 23 washauri wa polisi nchini Sudan Kusini wamekuwa wakihudhuria mafunzo mjini Juba ya jinsi ya kuhakikisha watoto wanalindwa katika taifa hilo lililoghubikwa na vita.

Maafisa hao wametoka katika majimbo 10 na wanahudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaojumuisha polisi UNPOL. Maafisa hao wanasema wakirejea katika majimbo yao watahakikisha wanatekeleza kwa vitendo waliyon’gamua.

Paul Mwangi raia wa Kenya anayefanya kazi na UNPOL, ni miongoni mwa wanaoshiriki mafunzo hayo kutoka jimbo la Rumbek. Amezungumza na Joshua Mmali mratibu wa mawasiliano wa UNMISS na kumueleza hali ya  Rumbek ilivyo.

(PAUL MWANGI CLIP)