Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na habari njema, hatua zaidi zahitajika kuinusuru dunia:UNEP

Mkulima nchini Thailand akiwa katika shamba lake la mpunga
David Longstreath/IRIN
Mkulima nchini Thailand akiwa katika shamba lake la mpunga

Pamoja na habari njema, hatua zaidi zahitajika kuinusuru dunia:UNEP

Tabianchi na mazingira

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s unaipeleka dunia katika mwelekeo unaopaswa lakini bado juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha malengo hayo yanatimia hususan yanayohusiana na mazingira na mabadiliko ya tabianchi. 

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Erik Solheim, akizungumza na UN News na kutolea mfano nyangumi aliyemeza mifuko 80 ya plastiki iliyotupwa kwenye mwambao wa Thailand na kupoteza maisha.

Ameongeza kuwa ingawa ulinzi wa mazingira sio kitu kinachohitaji akili, mkasa huo unadhihirisha kibarua cha utunzaji wa mazingira bado ni kigumu na uwjibikaji unahitajika ili kuilinda dunia na wakazi wake.

Hata hivyo Bwana. Solheim amesema habari njema ni kwamba watu na serikali wameanza kuelewa na wanachukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi

(SAUTI YA ERIK SOLHEIM )

‘Ni muhimu sana kama wanadamu kakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kusitisha ongezeko la kasi la joto duniani, tuko njiani kutimiza hilo kwa maana kwamba tunayofanya tunaelekea katika njia sahihi na mwaka jana umekuwa mwaka wa kwanza katika historia ya mwanadamu tumekuwa na upatikanaji zaidi wa umeme duniani unaotokana na nishati ya jua kuliko jumla ya umeme wote utokanao na mafuta, gesi na makaa ya mawe.”

Amesema hata hivyo hatupaswi kubweteka kwani

( SAUTI YA ERIK SOLHEIM )

“Kasi ni ya muhimu sana, ndio tuko katika msitari lakini ni lazima tuongeze kasi, kuna habari nyingi nzuri lakini hazitoshelezi kuikoa dunia hivyo tunahitaji jitihada zaidi.”