Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kasi ya maisha inawasahau wazee-Dkt.Wachira

Idadi ya wazee. Picha: UM

Kasi ya maisha inawasahau wazee-Dkt.Wachira

Haki za binadamu

Usemi usemao “ya kale ni dhahabu” waonekana kupitwa na wakati, sio tu katika familia ambazo kwa miaka nenda miaka rudi zimekuwa zikiamini wazee ndio dhahabu inayoshikilia jamii kwani kadri wanavyozeeka ndivyo wanaongeza maarifa watakayoavichia vizazi vya sasa na vijavyo hususan barani Afrika.

Hayo ni kwa mujibu wa Dkt. Florence Wachira kutoka tume ya kitaifa nchini Kenya inayohusika na usawa wa kijinsia, usawa kwa ajili ya makundi yanayotengwa katika jamii ikiwemo wazee na jamii zilizotengwa, kandoni mwa mkutano wa wazi wa kuhusu masuala ya wazee unaondelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amesema kasi ya maisha imebadilika na hivyo…

(Sauti ya Dkt.Florence)

Na je  Kenya imeweka mikakati gani kulinda kundi hili adhimu katika jamii?

(Sauti ya Dkt. Florence)