Tume ya kuchunguza yaliyojiri katika maandamano ya Gaza 2018 yateuliwa:UN

25 Julai 2018

Watu watatu wameteuliwa na baraza  la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa katika jopo maalum litakalochunguza  yaliyojiri katika maandamano ya mwaka 2018 kwenye maeneo yanayokaliwa ya Palestina.

Jopo hilo lililotangazwa leo mjini Geneva Uswisi na  rais wa  baraza la haki za , balozi Vojislav Suc linajumjuisha David Michael Crane raia wa Marekani, Sara Hossain kutoka Bangladesh  na Kaari Betty Murungi wa Kenya, na jopo hilolitaongozwa na Bw Crane.

Uamuzi wa baraza hilo kuunda na kutuma haraka, tume huru ya uchunguzi ya  kimataifa  ulipitishwa katika kikao maaluma  cha Mei 18 mwaka 2018, ili, “kuchunguza madai yote ya ukiukwaji na kwenda kinyume na sheria  za kimataifa za haki za binadamu katika maeneo yanayokaliwa ya  Palestina  pamoja na eneo la Mashariki mwa Jerusalem, hususan katika ukanda wa Gaza kuhusiana na  mashambulio ya kijeshi yaliyofanywa dhidi ya wandamanaji ambao ni raia, maandamano ambayo yaliyoanza machi 30 mwaka 2018.”

Baraza la haki za binadamu, lenye wanachama 47,kwa kuingatia azimio namba S-28/1, llimelipa jukumu jopo hilo maalum, kwa kushirikiana na  wataalam husika kufuata utaratibu maalum, ili kutafuta ukweli na jinsi ya madai ya ukikwaji yalivyotekelezwa.

Photo/UNRWA
Nyumba ya familia ya Palestina katika ukanda wa Gaza ilibomolewa na watawala wa Israel

 

 Uchunguzi wao pia utahusu yale yanayoweza  kuwa “uhalifu wa kivita”na “kuwabaini waliohusika”.

Jopo hilo ambalo litafanya kazi huri limeombwa  na baraza  kutoa mapendekezo ya hatua za uwajibikaji kwa lengo la kukomesha ukwepaji wa sheria.

 Jopo hilo lintarajiwa kuwasilisha uchuguzi wake wa maneno kwa baraza hilo kwenye kikao chake cha 39 cha Septemba  2018 na ripoti ya mwisho yamaandishi katika kikao cha 40 kitakachofanyika Machi 2019.

 

Save the Children/Mohamed N Ali
Ghasia huko Gaza zilianza tarehe 30 mwezi Machi mwaka huu na mtoto huyu ni miongoni mwa majeruhi wa ghasia hizo.

 

Wanajopo hao wana uzoefu wa kutosha katikamasuala ya haki a sheria, mwenyekiti David Michael Crane ni mtaalamu wa masuala ya sheria za kimataifa na amefanya kazi kwa kipindi cha miaka zaidi ya 30 katika serikali ya Marekani. Amewahi kushika wadhifa wa mkaguzi mkuu katika wizara ya ulinzi ya Marekani. Kuanzia Aprili 2002 hadi 15 Julai 2005 alikuwa mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama maalum nchini Sierra Leoneiliyomuhukumu rais wa zamani wa Liberia ,Charles Taylor.

 Kaari Betty Murungi ni raia wa Kenya, wakili ambae amefanya kazi ngazi yakitaifa, kikanda  na pia  kimataifa na kushika nyadhifa za uongozi katika asasi mbalimbali zisizo za serikali. Aliwahi kufanya  kazi katika bodi ya  tume ya haki za binadamu ya Kenya  na pia katika  mahakama ya kimataifa iliyohusika na mauajiya kimbari ya Rwanda.

Na wakili Sara  Hossain ni raia wa Bangladesh ambako ameshika nyadhifambalimbali na kisha akateuliwa na tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu  kuwa mmoja wa wataalam kuhusu uwajibikaji kwa masuala yaKorea Kaskazini au DPRK.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter