Baada ya miaka 6 Tanzania yaaga UNBOA na kukabidhi ujumbe kwa Chile

25 Julai 2018

Tanzania imemaliza muda wake wa miaka sita wa kuwa mjumbe wa Bodi ya ukaguzi wa hesabu ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) na kukabidhi kijiti hicho kwa nchi ya Chile.

Tanzania  iliteuliwa  na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kuchukua nafasi hiyo tarehe 1 Julai, 2012.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Profesa Mussa Juma Assad ambae ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CAG)  , amsema Tanzania inaingia katika historia ya dunia kuwa ni nchi ya kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuwa mjumbe wa Bodi ya (UNBoA) na ni nchi ya tatu barani Afrika kuingia katika Bodi hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1946 na kuongeza kuwa

(Sauti ya Pro. Mussa Juma Assad)

Na je changamoto walizobaliana wakati wa kazi hiyo ngumu zimewajenga vipi?

(Sauti ya Pro. Mussa Juma Assad)

Kwa miaka hiyo sita Tanzania imewasilisha jumla ya ripoti 13 za ukaguzi wa mashirika na ofisi za Umoja wa Mataifa zikiwemo mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari kwa Yugoslavia ya zamani ICTY,  shirika la Idadi ya watu duniani UNFPA, la kuhudumia watoto UNICEF, la mpango wa maendeleo UNDP na la misaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter