Watu wenye ulemavu wahusishwe katika juhudi za kuwaendeleza:Amina

24 Julai 2018

Ahadi za serikali mbalimbali kuheshimu haki za watu wenye  ulemavu zimeimarishwakufuatia kupitishwa kwa ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa  na pia kutokana kuwepo kwa mkataba wa Umoja wa mataifa  kuhusu haki za watu wenye ulemavu kuidhinishwa na kuingia katika vipengee vya haki za binadamu mkataba ambao kwa sasa umeridhiwa kote duniani.

Hayo yamesemwa  na Naibu Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Bi Amina J.Mohammed, hii leo mjini London Uingereza wakati wa mkutano kuhusu watu wenye ulemavu.   

Bi. Mohammed amesema kwa masikitiko ahadi hii ya kisiasa mara kadhaa inapuuzwa hususani  kwa maisha ya watu takriban milioni 1.5 wenye ulemavu duniani.

Ameongeza kuwa wengi wa watu hao, bila kujali wapi waliko pamoja na uwezo wao bado wanabaguliwa  na, hasa katika mataifa yanayoinukia  na kuwakosesha haki zao zamsingi kama vile elimu, huduma za afya na pia kunyimwa haki ya kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Bi. Amina amesema mkutano huo ni fursa nzuri ya kutafuta njia za kubadili hali hiyo wakati huu wa utekelezaji wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu  kwakuwajumuisha watu wenye ulemavu.

 

Kundi la watoto kutoka chama cha watu wenye ulemavu katika kambi ya Khan Yunis wakicheza.
2016 UNRWA Photo by Hiba Kreizim
Kundi la watoto kutoka chama cha watu wenye ulemavu katika kambi ya Khan Yunis wakicheza.

Akiunga mkono hoja hiyo katika mkutano , mratibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya binadamu OCHA, Mark Lowcock, amesema wakati huu kuna changamoto kubwa  za hatua za kuhakikisha mahitaji ya kibinadamu  yanaweza kumfikia kila mtu kwani hivi sasa watu zaidi ya milioni 130 duniani  wanahitaji msaada wa kibinadamu na  asilimia 15 ya watu hao ni wenye ulemavu, hivyo akatoa rai ,“tutaomba msaada kutoka katika mashirika ya watu wenye ulemavu ili kuhakikisha kuwa masuala ya watu wenye ulemavu yanajumuishwa katika kila ngazi ya mipango ya kibinadamu.”

Pia amesema migogoro mbalimbali pamoja na  mabadiliko ya tabia nchi , vimesababisha  watu zaidi ya milioni 30 kuachwa bila makazi na kati ya hao theluthi moja ni watu wenye ulemavu.

Kwa mantiki hiyo amesema,  watu wenye ulemavu wanahitaji kupewa sauti ili waweze kutambua mahitaji yao wenyewe  na kuahidi kuwa ofisi yake itashauriana na makundi ya watu wenye ulemavu ili kuhakikisha kuwa  masuala yanayaowahusu yanajumuishwa katika  mipango ya utoaji wa misaada ya kibinadamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter