Zimbabwe ni lazima kuheshimu haki zabinadamu wakati wa uchaguzi:UN

Uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe unakaribia na wito umetolewa leo kwa wadau wote serikali, vyama vya kisiasi na wafuasi wao kuhakikisha kuwauchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya amani, utulivu , kuzingatia haki za binadamu na utawala wa sheria.
Wito huo umetolewa mjini Geneva Uswisi na na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikisisitiza kuruhusu maandamano na mikusanyiko ya amani. Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi za haki za binadamu,OHCHR, Bi Liz Throssel, uchaguzi huo umepangwa kufanyika Julai 30 na na maandalizi yanaendelea vyema
(SAUTI YA LIZ THROSSELL)
“Inaleta matumaini kuona mikutano ya hadhara na maandamano ya amani vinafanyika mjini Harare pamoja na matamshi ya uangalifu ya asasi za kiraia yenye matumaini mema. Kuwepo kwa baadhi ya makundi ya haki za binadamu ya kimataifa, mbali ya tume ya haki za binadamu ya Zimbabwe na tume ya jinsia ya Zimbabwe kufuatilia mazingira ya haki za binadamu kuelekea uchaguzi wa taifa ni ishara inayokaribishwa.”
Hata hivyo amesema wana wasiwasi na ripoti zinazodizi kusambaa kutoka mikoani ambapo baadhi ya wapiga kura wanatishiwapamoja na watu kulazimishwa kwenda katika mikutano ya kampeini. Kana kwamba hiyo haitoshi
(SAUTI YA LIZ THROSSELL)
“Pia kumekuwa na matumizi mabaya ya lugha dhidi ya wagombea wa viti vya wanawake. Tunaomba wakuu na vyama vya kisiasa na wafuasi wao kuhakikisha kuwa uchaguzi hauvurugwi na visa kama hivyo ili raia wote wa Zimbabbwe waweze kushiriki bila uoga katika mchakato wa uchaguzi wa kuaminika.”
Amekumbushia ahadi ya Juni 26 ambapo vyama vya kisiasa, chini ya tume ya amani na maridhiano ya taifa nchini humo vilitia saini makubaliano ya kudumisha amani wakati wa kampeini na uchaguzi. Huu ni uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia unafanyika Zimbabwe baara ya Rais muasisi wa Taifa hilo Robert Mugabe kushinikizwa kuachia ngazi mwishoni mwa mwaka jana.