Uongozi shupavu wahitajika kuzuia maambukizi mapya ya ukimwi:UNAIDS

24 Julai 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limezitaka nchi kuchukua hatua madhubuti ili kushughiulikia mgogoro wa kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi au VVU.

Kwa mujibu wa shirika hilo takriban watu wapya milioni 1.8 wameambukizwa VVU mwaka 2017 na nchi 50 zinakabiliwa na ongezeko la maambukizi mapya wakati huduma za kuzuia hazitolewi katika kiwango kinachostahili au hazitoshelezi.

 

World Bank/Arne Hoel
Uchunguzi wa virusi vya HIV

Akizungumza katika baraza kuu la ukimwi duniani linaloendelea mjini Amsterdam Uholanzi, mkurugenzi mtendaji wa UNAID  Michel Sidibé, amesema “Afya ni haki ya binadamu , na tunatiwa hofu na ukosefu wa ari ya kisiasa na kushindwa kuwekeza katika mipango ya ukimwi, hususan kwa vijana na makundi muhimu katika jamii. Endapo nchi zinadhani zitaweza kuepuka janga hili bila hayo basi zimebugi stepu.”

Ripoti mpya iliyotolewa na UNAIDS , “Safari ndefu:kuziba mapengo, kuondoa vizuizi, kuondoa kutokuwepo haki, inaonyesha kwamba asilimia 40 ya maambukizi mapya ya VVU kote duniani ni miongoni mwa makundi muhimu. Ingawa mchanganyiko wa mbinu za kupambana na ukimwi umesaidia kwa baadhi ya makundi, ikiwemo kupungua kwa vitendo vya watu kujizuru, huduma ya mipira ya kujikinga kama condomu, nchi nyingi haziko tayari kuwekeza katika mitazamo ambayo inaonekana kama ni kinyume na utamaduni au misingi ya dini, isiyo na umaarufu au inayopinga sheria mbaya zilizopo katika nchi fulani.

 

Trinn Suwannapha / World Bank
Mtoa huduma wa kujitolea akitoa sindano safi kwa watumiaji mihadarati nchini Thailand

UNAIDS inasema maambukizi ya VVU yanaweza kuwa ya juu hadi asilimia 70 miongoni mwa makahaba katika baadhi ya nchi zilizoko Kuisni mwa Afrika , hata hivyo karibu robo tatu ya nchi zinazoripoti kwa UNAIDS kuharamisha ukahaba na makahaba , zinasema kwamba mara nyingi mipira ya kujingika au kondomu huchukuliwa na polisi.

Kwa Mashariki mwa Ulaya na Asia ya Kati , theluthi moja ya maambukizi mapya ya VVU yamo miongoni mwa watu wanaojidunga dawa za kulevya, asilimia 87 ya nchi zinazoripoti kwa UNADS kuharamisha matumizi au kuwa na dawa za kulevya , kunawafanya watu kujificha na kukosa kufika kwenye huduma za VVU.

Nchi nyingi hazihakikishi usalama wa sindano zinazotumika na kuwa na vituo vinavyotoa huduma mbadala ya matumizi ya mihadarati , hali ambayo ni kikwazo kikubwa katika juhudi za kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa jamii hizo za watumiaji wa mihadarati na wenzi wao.

TAGS:UNAIDS, VVU, maambukizi, Michel Sidibe.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter