Biashara ya utumaji pesa kupitia mitandao si mali ya serikali-UNCTAD
Huduma ya mfumo wa kupokea pesa kutoka ughaibuni kupitia teknolojia ya mitandao na apu mbalimbali inazidi kushika kasi barani Afrika na katika mataifa mengine yanayoinukia imesema kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo na biashara UNCTAD.
Kwa mujibu wa UNCTAD huduma hiyo imesaidia sana mamilioni ya watu wa masikini ambao hupokea fedha kutoka kwa jamaa zao walioko ughaibuni. Hata hivyo huduma hiyo inaanza kukukabiliwa na changamoto kufuatia baadhi ya serikali kuweka kodi kubwa katika biashara hiyo,jambo ambalo limezusha mjadala mkali.
Dkt Mukhisa Kituyi, ni Katibu Mkuu wa UNCTAD,akiwa kwenye mkutano wa maendeleo endelevu mjini New York Marekani alizungumzia suala hilo.
(SAUTI YA MUKHISA KITUI )
Na kuhusu mipango ya mataifa ya Afrika kuwa na sarafu moja amesema
(SAUTI YA MUKHISA KITUI )