Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India sheria yenu dhidi ya usafirishaji  haramu wa watu iende sanjari na haki za binadamu :UN

IOM
Usafirishaji haramu wa watoto. Picha: IOM

India sheria yenu dhidi ya usafirishaji  haramu wa watu iende sanjari na haki za binadamu :UN

Haki za binadamu

Serikali ya India imeshauriwa kudurusu  tena sheria yake mpya yenye nia ya kukabiliana na usfirishaji haramu wa binadamu  ili kuhakikisha hatua zinazopendekezwa zinakwenda sanjari na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Ushauri huo umetolewa leo mjini Geneva Uswisi na wataalamu wawili wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Wataalam hao wanasema wanatiwa hofu na muswada wa sheria hiyo kama ulivyowasilishwa bungeni na serikali ya  India  Julai 18 kwani unatilia mkazo zaidi sheria za jinai kukabiliana na tatizo hilo lakini hautoshelezi katika haki za binadamu hasa kwa upande wa mahitaji ya waathirika na ulinzi wao ama huduma  wanazopaswa kupata hali ambayo inaongeza hatari kwa watu ambao yatari wako katika hali mbaya.

Wameongeza kuwa usafirishwaji haramu wa binadamu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na wamelihimiza bunge la India kutathimini tena sheria hiyo na kuzingatia utaratibu wa misingi ya mapendekezo ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR kuhusu usafirishaji wa binadamu.