Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupunguza hasara za kiuchumi zitokanazo na majanga kutabadili maisha:UN

Majanga kama haya ya mafuriko Sudan Kusini huwa na madhara kiafya: Picha: UN-Photo-Isaac-Bill

Kupunguza hasara za kiuchumi zitokanazo na majanga kutabadili maisha:UN

Tabianchi na mazingira

Kuweza kupungunza hasara za kiuchumi zitokanazo na majanga ynayochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi  kutasaidia kubadili maisha ya mamilioni ya watu umesema Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kwa ajili upunguzaji wa athari za majanga Mami Mizutori, “hasara za kiuchumi zitokanazo na mjanga kwa mataifa ya kipato cha chini na cha wastan zinaathiri juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s, na kuzinyima nchi fedha za kutumia katika masuala mengine kama afya, elimu, usatawi wa jamii na mahitaji mengine muhimu ya jamii.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji wa athari za majanga UNISDR, inasema kila mwaka majanga yanaugharimu uchumi wa dunia takriban dola bilioni 250, yanawantawanya mamilioni ya watu na kuwatumbukiza wengi katika umasikini.

Hivyo kupunguza hasara hizo kuna uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha ya watu na hiyo itakuwa kaulimbiu ya     mwaka huu katika siku ya kimataifa ya upunguzaji majanga hapo Oktoba 13.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo wa kampeni zaba za mkutano wa Sendai ambazo hutumia siku ya kimataifa ya upunguzaji athari za majanga kupigia upatu malengo 7 ya mkutano wa Sendai yaliyoafikiwa 2015-2030 ya kupunguza hasara za kiuchumi zitokanazo na majanga kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Kujikita katika suala hili kutawasaidia watunga sera na wawekezaji wa miundombinu kuelewa umuhimu wa kuhakikisha uwekezaji huo unatambua hatari zilizopo.

UNISDR inasema endapo hawatatambua hatari zilizopo upunguzaji huo hautokua endelevu, na kama sio endelevu basi utakuwa na harasa kwa watu, na hasara hizo ni dhahiri kwa kiwango cha watu wanaotawanywa na majanga kote duniani.

Mwaka jana pekee takriban watu milioni 18 walitawanywa na matukio yaliyosababishwa na mjanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.