Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maombi ya kushiriki mtihani wa (YPP) 2018 kwa vijana waliobobea kitaaluma

Bendera ya Umoja wa Mataifa
Picha: UM/Mark Garten
Bendera ya Umoja wa Mataifa

Maombi ya kushiriki mtihani wa (YPP) 2018 kwa vijana waliobobea kitaaluma

Masuala ya UM

Kila mwaka, Umoja wa Mataifa hutafuta vijana waliobobea katika fani mbali mbali, ambao wapo tayari kuanza huduma ya kitaaluma kama wahudumu wa kimataifa wa umma. Mpango wa Vijana Waliobobea Kitaaluma, yaani YPP, huleta vipaji vipya kwa Umoja wa Mataifa kupitia mtihani wa kila mwaka.

Ili kupata fursa ya kushiriki mtihani huu, ni lazima uwe unatoka nchi zilizoorodheshwa kushiriki mwaka 2018, uwe na shahada ya kwanza, uwe unaongea Kiingereza au Kifaransa sanifu, na uwe na umri wa miaka 32 kabla ya mwisho wa mwaka huu. Utatakiwa kufanya ombi la kushiriki mtihani huu kabla ya tarehe 9 Agosti 2018.

Kumbuka, itakuwa vyema ikiwa utakamilisha na kuwasilisha maelezo yote kwa njia sahihi na nadhifu kwani hicho kitakuwa kigezo cha kupima uwezo wa wako kukubaliwa kuufanya mtihani.

Kumbuka pia kuwa, maombi ambayo hayatakamilishwa vyema au yatakayochelewa kuwasilishwa hayatakubaliwa, kwa hiyo ni lazima uwasilishe ombi lako kabla ya tarehe ya ukomo.

Kuona kama nchi yako inashiriki, na maelezo zaidi, tembelea tovuti

http://bit.ly/1aAemgZ