Skip to main content

Manusura wa kujilipua ageuka mtoa msaada wa sheria kwa wasichana

Bol  nchini Chad, wakati wa ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed (kushoto) akizungumza na Halima Yakoy Adam ambaye ni manusura wa shambulio alilopangiwa kufanya na Boko Haram
UN News/Daniel Dickinson
Bol nchini Chad, wakati wa ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed (kushoto) akizungumza na Halima Yakoy Adam ambaye ni manusura wa shambulio alilopangiwa kufanya na Boko Haram

Manusura wa kujilipua ageuka mtoa msaada wa sheria kwa wasichana

Amani na Usalama

Msichana mmoja nchini Chad ambaye alinusurika kuuwa na bomu alililobebeshwa na Boko Haram ili kufanya mauaji, ameamua kuwa mtoaji wa msaada wa sheria kwa  kwenye ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA huko Bol nchini Chad. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Huyu ni Halima Yakoy Adam binti wa miaka 18 ambapo miaka mitatu ambaye anasema akiwa na umri wa miaka 15  alilaghaiwa na mumewe ambaye ni mvuvi na mfuasi pia wa Boko Haram ..

“Nilidanganywa, waliniambia kuwa tunaenda kambi ya uvuvi lakini walinipekela eneo la Boko Haram, tulitumia siku tatu kabla ya kufika. Tulikaa hapo kwa mwaka mmoja.”

Halima alikuwa anatoa simulizi hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed wakati wa ziara yake huko nchini Chad hivi karibuni akisema kuwa hivi sasa wameachana na mumewe na hajui aliko.

Akizungumza bila hofu, Halima anasema baada ya mafunzo kwa mwaka mmoja, Halima pamoja na wasichana wengine wawili walitakiwa kubeba mabomu na kwenda kujilipua kwenye soko la wiki mjini Bol ili kuua watu na kuwatia wengine ulemavu na lengo ni kuwatia hofu wananchi.

Hata hivyo Halima anasema siku hiyo ya tarehe 22 Disemba 2015, mpango huo ulivurugika kwani maafisa wa usalama waliwabaini wasichana hao watatu na kujaribu kuwakamata..

“Tulikaa kwenye kisiwa kimoja kwa siku mbili ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya soko la wiki, nilikuwa nasali, nikiwa na bomu ndani ya mfuko wa plastiki, wasichana wawili walilipua bomu lao walifariki dunia, bomu langu lililipuka lakini nilikuaw salama ingawa miguu yangu miwili ilikatika.”

Hivi sasa Halima amepona na amepatiwa mafunzo ya kutoa msaada wa sheria kwenye kituo cha UNFPA mjini Bol na anatumia mfano wa mapito yake ili kuwatahadharisha wasichana hatari za misimamo mikali pamoja na haki zao za msingi.