Poland hakikisheni magereza yanatumiwa vyema UN
Poland imesonga mbele katika kuimarisha mazingira ya maeneo ya kuweka vizuizini watuhumiwa nchini humo lakini hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kuimarisha zaidi, ikiwemo hatua za ulinzi na kuepusha matumizi holela ya kutumia vizuizi hivyo.
Ushauri huo umetolewa leo mjini Warsaw Poland na wajumbe wa kamati ndogo ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia mateso wakati wakiwasilisha mbele ya mamlaka za nchi hiyo ripoti yao ya awali ya siri kuhusu jinsi ya kuimarisha ulinzi wa watu walionyimwa uhuru wao kutokana na mateso, ukatili na vitendo visivyo ya kibinadamu.
Kiongozi wa ujumbe huo Bi Aisha Shujune Mohammad amesema ingawa wanapongezahatua za Poland lakini bado ichukue hatua zaidi kwenye haki za msingi za ulinzi.
Pia wamesema wanaamini kwamba matumizi ya mbadala wa kizuizi yatapunguza idadi ya watu walioko korokoroni na hivyo kuboresha mazingira ya maeneo hayo.
Ujumbe huo ulitembelea sehemu mbalimbali kunakozuliwa watu na kupata kwa undani jinsi mfumo wa vituo vya magereza ulivyo kwa sasa.
Kamati hiyo huwa inachunguza jinsi mataifa yaliyoridhia itifaki ya mkutano dhidi ya utesaji-OPCAT yanavyotekeleza majukumu yao ya mkataba huo pamoja na kuunda mfumo huru wa kitaifa kuhusu uzuaji.
Poland illiridhia itifaki hiyo mwaka 2005.