Mvutano wa China na Marekani waumiza Afrika-UNCTAD

Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi.(Picha:UM/Jean-Marc Ferre)

Mvutano wa China na Marekani waumiza Afrika-UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Msemo ya kwamba wapiganapo mafahali wawili ziumiazo nyasi umedhihirika baada ya mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na China kusababisha ongezeko la gharama ya bidhaa na hivyo kuathiri mataifa ya Afrika.

Akihojiwa na idhaa hii mwishoni mwa mwa jukwaa la ngazi ya juu kuhusu maendeleo endelevu, SDGs jijini New York Marekani, Katibu Mkuu wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, Dkt Mukhisa Kituyi ametaja jinsi mataifa ya Afrika yanavyoathirika.

 

(SAUTI YA MUKHISA KITUYI)